• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 7:53 PM
Vibanda vya mahasla kujitafutia riziki vyabomolewa South B

Vibanda vya mahasla kujitafutia riziki vyabomolewa South B

NA SAMMY KIMATU

ZAIDI ya vibanda 600 vimebomolewa Alhamisi asubuhi katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Sokoni, South B, kaunti ndogo ya Starehe jijini Nairobi.

Akiongoza operesheni hiyo, msaidizi wa kamishna katika tarafa ya South B, Bw Solomon Muranguri amesema nia ya ubomoaji huo ni kuwaondoa wafanyabiashara wote walionyakua sehemu ya barabara ya watu kupitia.

Bw Muranguri aliongeza kwamba sababu nyingine ni kwamba waathiriwa waliziba mitaro ya kupitisha majitaka huku serikali ikichukua taadhari za mapema kukabiliana na mvua ya El Nino ambayo Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa ilitangaza inatarajiwa kuanzia Oktoba 2023.

Vibanda vyabomolewa huku wafanyakazi wa serikali ya kaunti (NCC) wakifagia na kuzoa taka. PICHA | SAMMY KIMATU

Msako wetu unashirikisha maafisa wa utawala (NGAO), serikali ya kaunti (NCC) sawia na polisi.

“Shughuli hii inahusisha idara kadhaa za serikali pamoja na kikosi cha maafisa wa kukabiliana na majanga katika kaunti ndogo ya Starehe kikiongozwa na naibu kamishna wa kaunti eneobunge la Starehe, Bw John Kisang,” Bw Muranguri akasema.

  • Tags

You can share this post!

Programu ya kutatua migogoro kidijitali yazinduliwa nchini

Seneta Sifuna amkashifu ‘Mtoto Wa Maumau’...

T L