• Nairobi
  • Last Updated April 17th, 2024 5:55 PM
Wagonjwa wa figo Lamu taabani, wahamishiwa Mombasa

Wagonjwa wa figo Lamu taabani, wahamishiwa Mombasa

NA KALUME KAZUNGU

WAGONJWA wa figo wanaotegemea hospitali ya King Fahd mjini Lamu, wameghadhabishwa na hatua ya kaunti kukifunga kitengo cha kusafisha na kutibu figo ambacho ndicho tegemeo lao la kipekee.

Serikali ya Kaunti ya Lamu imefunga kitengo hicho kwa muda usiojulikana, baada ya mtambo wa kusafisha maji kwa matumizi ya kimat – ibabu kuharibika kwa wiki kadhaa sasa na kutatiza huduma.

Wagonjwa wote 15 wa figo waliokuwa wakitegemea hospitali hiyo wamepewa rufaa hadi hospitali mbalimbali zilizo Mombasa.

Warsami Nuno Mahmoud, 74, alilalamika wamekuwa wakirudishwa nyumbani bila kutibiwa hata kabla tatizo la maji kuanza.

“Leo ni siku ya 12 bila kusafishwa figo zangu. Nimepewa rufaa kwen – da hospitali ya kibinafsi Mombasa.

Sina fedha za usafiri wala mahali pa kuishi. Itabidi nijikaze kuomba wahisani la sivyo nitalemewa na hali yangu,” akasema Bw Mahmoud.

Said Hussein, 50, ambaye ni mkazi wa Ndambwe, Wadi ya Mkunumbi, anasema aliamua kuishi kisiwani Lamu tangu 2019 alipogunduliwa ana maradhi ya figo yaliyohitaji apokee huduma ya kusafishwa figo mara mbili kwa wiki na sasa hana namna.

Naye Mohamed Ali Mzee, 63, alisema hawezi kumudu gharama ya usafiri na pia mahali pa kuishi wakati akitibiwa mjini Mombasa.

“Ombi letu ni kaunti ituzingatie. Sina fedha na sioni mbele kutakuwaje,” akasema Bw Mzee.

Waziri wa Afya katika Kaunti ya Lamu, Bi Anne Gathoni, alisema hatua hiyo imechukuliwa ili kutoa nafasi ya ukarabati wa kina kurekebisha tatizo lililopo kabla ya huduma kuendelea kutolewa.

“Mashine zetu zote za kusafisha fi – go ziko sawa. Changamoto iliyopo ni upande wa maji. Tumejaribu kurekebisha mtambo wa kusafisha maji lakini tatizo linajirudiarudia.

Ndio sababu tukaamua kuwapa wagonjwa wetu rufaa kwenye hospitali za Mombasa,” akasema Bi Gathoni.

Kitengo cha matibabu ya figo kwenye hospitali ya King Fahd mjini Lamu kilibuniwa na kufunguliwa mwaka 2018 kupitia mpango wa serikali ya kitaifa wa kufadhili mashini za matibabu kwa kaunti (MES).

  • Tags

You can share this post!

Uhaba wa maziwa wakumba Kisumu

Mudavadi achemkia Uhuru kwa madai Ruto alitaka...

T L