• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 6:07 PM
Waititu, mkewe Susan wana kesi ya kujibu katika kashfa ya Sh588m za ujenzi wa barabara

Waititu, mkewe Susan wana kesi ya kujibu katika kashfa ya Sh588m za ujenzi wa barabara

NA RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA ya kuamua kesi za ufisadi imeamua aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu, mkewe Susan Wangari na washtakiwa wengine wako na kesi ya kujibu katika kashfa ya ujenzi wa barabara kwa gharama ya Sh588 milioni.

Katika uamuzi wake, hakimu mkuu Thomas Nzioki alisema mashahidi 32 waliofika kortini walitoa ushuhuda uliowahusisha Waititu na wenzake na ubadhirifu huo wa pesa katika Kaunti ya Kiambu alipokuwa gavana.

Akiwaamuru washtakiwa wajitetee kabla ya hukumu kupitishwa, Bw Nzioki alisema, “Baada ya kutathmini ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka, nimefikia uamuzi kwamba kuna ushahidi wa kutosha kuwezesha mahakama kuwaweka washtakiwa kizimbani kujitetea.”

Akiomba hakimu amwachilie, Waititu alisema alifunguliwa na mashtaka kwa kuunga mkono mrengo wa kisiasa wa Rais William Ruto.

Waititu alieleza mahakama alitofautiana na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, ndipo akaagiza ashtakiwe.

Waititu na mkewe Susan Wangari pamoja na kampuni ya Saika Two Estate Developers Limited walikabiliwa na shtaka la kupokea kitita cha Sh25 milioni za ukarabati wa barabara kutoka kwa kampuni ya Testimony Enterprises Limited Contractor.

Mahakama ilisema utoaji zabuni za ujenzi wa barabara katika kaunti ya Kiambu ulikinzana na sheria.

  • Tags

You can share this post!

Ugaidi: Fahamu kwa nini ni ‘makosa’ kuzaliwa...

Mlima Kenya walia kupanda kwa gharama ya maisha licha ya...

T L