• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Wakili ataka TI Kenya itoe hoja nzito za kumpokonya Haji tuzo ya Uadilifu

Wakili ataka TI Kenya itoe hoja nzito za kumpokonya Haji tuzo ya Uadilifu

Na RICHARD MUNGUTI

KAMPUNI moja ya mawakili jijini Nairobi inataka shirika la kupambana na ufisadi la Transparency International (TI-Kenya) litaje sababu nzito za kumnyang’anya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji tuzo ya Uadilifu kwa masuala ya uongozi.

Kampuni ya Musyoki Mogaka kupitia kwa wakili Danstan Omari imemtaka mkurugenzi mkuu wa TI-Kenya Bi Sheila Masinde kutoa sababu za kutwaa tuzo hiyo.

Bw Omari amesema hatua ya kumnyang’anya tuzo hiyo inamdunisha Haji kwa lengo la kuhakikisha amekosa kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ujasusi.

Rais William Ruto alimteua Bw Haji kutwaa wadhifa wa mkurugenzi wa idara ya ujasusi.

Bw Omari amesema haki za Haji zimekandamizwa na TI na Bi Masinde kwa vile “wamempokonya tuzo hiyo bila kumwarifu ama kumpa muda ajitetee.”

Katika barua aliyoandikiwa Haji, Bi Masinde alisema tuzo hiyo inatwaliwa kwa sababu ametamatisha kesi nyingi zilizokuwa zinawakabili viongozi wanaodaiwa kuhusika kwa ufisadi.

  • Tags

You can share this post!

CAF yapokea rasmi azma ya Kenya, Uganda na TZ kutaka...

Chakula kibovu: Mpishi shuleni Mukumu afunguka

T L