• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 3:04 PM
Waziri Kindiki aonya Azimio kuhusu maandamano

Waziri Kindiki aonya Azimio kuhusu maandamano

NA MERCY KOSKEI

WAZIRI wa Usalama wa Ndani Prof Kithure Kindiki ametoa onyo kali kwa wanasiasa wanaochochea wananchi kushiriki maandamano.

Kulingana na Kindiki, wanasaisa wengi wanajificha kwa demokrasia ili kutenda mambo ambayo yanaleta msukosuko nchini akisema kuwa serikali haitaruhusu hayo.

Akizungumza katika kanisa la Kenya Assemblies of God (KAG) Sagana Town, Kaunti ya Kirinyaga Juni 4, 2023, Kindiki alisema kuwa nia ya serikali si kuingilia demokrasia ya Mkenya yeyote ambayo imeundwa na Katiba kwani kila mmoja ana uhuru wa kutoa maoni ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Akihutubia mamia ya waumini kwenye ibada iliyoongozwa na Mchungaji Faith Murimi, Waziri alisema kuwa serikali inataka kila mwanasiasa na Mkenya kuwajibika.

Akitoa onyo kali, Kindiki alisema serikali haitasaza wanaojificha chini ya uhuru wa kujieleza kwa minajili ya binafsi zao za kisiasa ili kusababisha machafuko na kuvuruga biashara za watu.

Waziri lisikitika kuwa wengi waliumia na mali yenye thamani kubwa kuharibiwa wakati wa maandamano ya Azimio Februari 2023, huku watu kadha wakipoteza uhai.

Akiwakikishia Wakenya, Kindiki alisemq idara ya usalama wa nchi haitakubali mwanasiaisa yeyote kutumia kisingizio kwamba ana uhuru kidemokrasia ilhali anakiuka sheria na kuvuruga amani.

“Kama vile tumeambia wahubiri, kwamba ukijificha kwa kanisa ama kwa Waislamu tutakutoa ulipo na kukufichua. Isitoshe, viongozi wa kisasa katika ngazi zote lazima wafanye siasa zao kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi ya Kenya,” Kindiki alisema.

Kauli ya Waziri Kindiki imejiri wakati ambapo mrengo wa upizani, Azimio unatishia kurejelea maandamano kufuatia jaribio la kupitishwa Mswada tata wa Fedha 2023.

Mswada huo unapendekeza nyongeza ya ushuru (VAT), kinara wa Azimio Bw Raila Odinga akitishia kushawishi wabunge wa upinzani kuangusha mswada huo.

Bw Raila ambaye pia ni kiongozi wa ODM, analalamikia mswada huo akisema utachochea gharama ya maisha kuwa juu mara dufu.

  • Tags

You can share this post!

Rais Ruto azuru Narok kushiriki sherehe kufurahia Waziri...

Dj Brownskin akamatwa kwa kusaidia mkewe kujitia kitanzi  

T L