• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 5:55 AM
Afrika Kusini yapiga kura ya kuvunja uhusiano na Israel kwa sababu ya ‘ukatili’

Afrika Kusini yapiga kura ya kuvunja uhusiano na Israel kwa sababu ya ‘ukatili’

NA MASHIRIKA

PRETORIA, AFRIKA KUSINI

WABUNGE nchini Afrika Kusini walipiga kura siku ya Jumanne kuunga mkono kufungwa kwa ubalozi wa Israel jijini Pretoria.

Aidha, walifanya hivyo kushinikiza kusimamishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia hadi makubaliano ya kusitisha mapigano yatakapokubaliwa katika vita vyake na kundi la Kiislamu la Palestina, Hamas, eneo la Gaza.

Azimio hilo kwa kiasi kikubwa litakuwa alama iliyowekwa kwani itakuwa juu ya serikali ya Rais Cyril Ramaphosa iwapo itatekeleza; msemaji wa ofisi ya rais alisema Ramaphosa “anakumbuka na kuthamini” mwongozo wa bunge kuhusu uhusiano wa kidiplomasia wa Afrika Kusini na Israel, hasa kuhusu hadhi ya ubalozi.

“Rais na Baraza la Mawaziri wanahusika katika suala hilo, ambalo linabaki kuwa jukumu la afisa mkuu mtendaji wa kitaifa,”Vincent Magwenya alisema.

Ramaphosa na maafisa wakuu wa wizara ya mambo ya nje wamekuwa wakikosoa vikali uongozi wa Israel wakati wa kampeni yake mbaya ya kijeshi dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza wenye wakazi wengi, wakiitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu kuwachunguza kwa uhalifu wa kivita unaoweza kutokea.

Hata hivyo, Ubalozi wa Israel haukujibu chochote kuhusiana na tukio hilo.

Fauka ya hayo, manmo Jumatatu wiki hii, Balozi wa Israel jijini Pretoria aliitwa tena Tel Aviv kwa mashauriano kabla ya upigaji kura, ambao siku ya Jumanne ulipitishwa kwa sauti ya juu huku matokeo yakiwa kura 248 dhidi ya kura 91.

Zaidi ya hayo, azimio hilo la bunge lililetwa na chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) wiki iliyopita wakati chama tawala cha African National Congress kilipoahidi kuunga mkono kile ambacho kimekuwa msimamo mkuu wa kidiplomasia kwa Afrika Kusini tangu Nelson Mandela awe rais wa kwanza kuwahi kuchaguliwa kidemokrasia katika nchi hiyo mnamo 1994.

Kiranja wa Wengi wa ANC, Pemmy Majodina, alirekebisha hoja ya mwisho ya rasimu ya azimio la EFF la kutaka ubalozi huo kufungwa na kusimamishwa kazi kwa njia ya kidiplomasia, na kujumuisha maneno haya: “… Mazungumzo yanayoratibiwa na Umoja wa Mataifa ambayo matokeo yake lazima yawe amani ya haki, endelevu na ya kudumu.”

Vilevile, EFF ilipendekeza hoja hiyo siku ya Alhamisi kwa mshikamano na watu wa Palestina kuhusu mashambulizi ya Israel kwa mabomu na uvamizi wa Gaza inayotawaliwa na Hamas, iliyochochewa na uvamizi mbaya wa wanamgambo wa Hamas ndani ya Israel mnamo Oktoba 7.

  • Tags

You can share this post!

Afafanua umuhimu wa kuzingatia kilimo asilia kwa kudumisha...

Afisa wa zamani wa magereza asubiri tambiko kabla ya...

T L