• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 8:50 AM
Ajuza wa miaka 70 akaidi sayansi na kujifungua mapacha

Ajuza wa miaka 70 akaidi sayansi na kujifungua mapacha

KAMPALA, Uganda

NA DAILY MONITOR

MWANAMKE mwenye umri wa miaka 70 ameshangaza wengi baada ya kujifungua pacha na kukaidi sayansi kwamba ni vigumu kwa mwanamke mwenye umri huo kuzaa.

Bi Safiina Namukwaya, mkazi wa Wilaya ya Masaka, Novemba 29, 2023 alijifungua mtoto wa kiume na wa kike wakiwa na uzito wa kilo 1.7 kila mmoja.

Alijifungua katika Kituo cha Kimataifa cha Uzazi cha Hospitali ya Wanawake ya Kampala ambako alikuwa amelazwa kwa siku tano kwa ajili ya maandalizi ya kujifungua katika chumba cha faragha.

“Kuna wakati niliugua sana kwa sababu ya ujauzito, nilitumia karibu pesa zangu zote. Nilitafuta huduma katika hospitali ya Kyabakuza na baadaye nikampigia simu Dkt Sali. Aliniambia nisafiri hadi Kampala lakini nikamwambia sina pesa hata kidogo na akanipangia jinsi ya kusafiri kwenda hospitali,” alisimulia.

Mumewe amemtelekeza.

“Wanaume hawapendi kuambiwa kuwa umebeba zaidi ya mtoto mmoja. Tangu nilipolazwa hapa, mume wangu hajawahi kuja kunijulia hali. Dkt Sali amegharamia kila kitu kana kwamba yeye ndiye baba wa watoto,” alisema.

Bi Namukwaya alisema aliamua kupata mimba baada ya kutukanwa kwa kukosa mtoto.

“Niliwalea watoto wa watu wengine na ningewaona wakikua na kuniacha peke yangu. Nilijiuliza ni nani angenitunza nitakapozeeka. Wakati mmoja, mvulana mdogo sana alipata kutoelewana na kunidhihaki, akisema nililaaniwa na mama yangu nifariki bila kujaliwa kuzaa mtoto,” aliongeza.

Mume wa kwanza wa Bi Namukwaya alifariki mwaka wa 1992.

Wakati wa ndoa, alikuwa na mimba iliyoharibika.

Miaka minne baada ya kufiwa na mumewe, aliingia kwenye uhusiano mwingine lakini bado hakuweza kuzaa watoto.

Alipoulizwa kuhusu utayarifu wake wa kuwatunza watoto hao, alisema: “Kwa kweli sijui, Mungu ndiye anayejua. Unaona, unaweza kupata mtoto mmoja na ukajihisi kulemewa lakini hapa niko na pacha wakati niko dhaifu, wakati ninashindwa kwenda kwenye shamba langu kulima chakula cha kuuza, sijui!…. wanasema kila mtoto huja na baraka zake.”

Bi Namukwaya ana mtoto mwingine mmoja, msichana, ambaye alizaliwa 2020.

Baada ya takriban dakika 40 akihojiwa na mwanahabari wetu, wauguzi walikuja kumchukua kujifungua.

Bi Namukwaya alitembea kwa ulegevu huku muuguzi akiendelea kuuliza jinsi alivyohisi.

Akimhudumia, Dkt Sali alisema umri ni idadi tu mbele ya teknolojia ya kisasa.

“Yeye sio wa kwanza. Tumefikisha zaidi ya wagonjwa 60 katika kipindi cha miaka 15 ambao wana umri wa zaidi ya miaka 50. Safiina alikuja hapa miaka mitatu iliyopita akiwa na umri wa miaka 67 na akaniambia amekuwa kwenye ndoa kwa miaka 40 na alikuwa akitaka mtoto. Nilimwangalia na kisha kumwambia, una umri mdogo kuliko Sarah wa Biblia (aliyezaa akiwa na miaka 90). Yawezekana,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Mbangladeshi alivyoporwa Dola 5, 000 kwa kukosa kulipia...

Mfuasi sugu wa Azimio ashtakiwa kumdhalilisha Rais Ruto

T L