• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 9:55 AM
Amerika yaadhibu spika wa Uganda kwa kupitisha sheria inayoharamisha ushoga na usagaji

Amerika yaadhibu spika wa Uganda kwa kupitisha sheria inayoharamisha ushoga na usagaji

NA MERCY KOSKEI

AMERIKA imefutilia mbali visa ya spika wa bunge la kitaifa wa Uganda Anita Among, baada ya kupitisha sheria za kutotambua mashoga na wasagaji nchini humo.

Kulingana Asuman Basalirwa, aliyewasilisha mswada huo, ujumbe huo wa kufutilia mbali visa ya sasa ya spika huyo ulithibitishwa kupitia barua pepe.

Akinukuu ujumbe huo baada Rais wa Uganda Yoweri Museveni, alipuuzilia mbali shinikizo kutoka kwa mataifa ya magharibi na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kutaka kuunga mkono mswada kupinga ushoga kuwa sheria.

“Taifa la Amerika limetupilia mbali visa ya spika wa Uganda. Kwa sasa Anita Among hana visa ya Anerika,” alisema huku akionyesha nakala ya barua pepe hiyo kwa wanahabari

Kulingana na Basalirwa, spika huyo amehimizwa kupeleka pasipoti yake kwa afisi za Ubalozi wa Amerika kupitia wizara ya mambo ya nje kwa ajili ya marekebisho ya visa yake.

“Nadhani walikuwa wanatafuta visa yangu lakini hawakuipata na hivyo mwathiriwa wa kwanza akawa spika,” alisema mbunge huyo wa manispa ya Bugiri.

Klulingana na sheria ya sasa  ya uganda, wale wanaoshiriki ushoga wanakabiliwa na adhabu kali ambayo inaweza kujumuisha kifungo cha maisha.

Siku ya Jumatatu, Mei 29, 2023 Among alitangaza kuwa  bunge  litasimama kidete  kukuza maadili ya watu wa Uganda.

“Sasa ninawahimiza watekelezaji wajibu chini ya sheria kutekeleza mamlaka waliyopewa katika Sheria ya kupinga Ushoga. Wananchi wa Uganda wamezungumza na ni wajibu wenu sasa kusimamia sheria kwa haki na udhabiti,” alisema kupitia mtandao wake wa Twitter.

 

  • Tags

You can share this post!

Nyumba Yangu: Wanariadha kunufaika kupitia ushirikiano wa...

Washtakiwa kwa wizi wa samaki

T L