• Nairobi
  • Last Updated April 15th, 2024 2:58 PM
Babu Owino aorodheshwa mbunge bora zaidi katika utendakazi

Babu Owino aorodheshwa mbunge bora zaidi katika utendakazi

Na WANGU KANURI

BABU OWINO, mbunge wa Embakasi Mashariki aliongoza orodha ya wabunge 20 walioratibiwa katika utendakazi wao miezi minane baada ya kuchaguliwa Agosti 2022.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Leeway Africa, viongozi hao walipigiwa debe na wakazi wa maeneo wanayoongoza huku Babu akiibuka nambari wani.

Mbunge huyo aliyevuma kupitia chama cha ODM aliongoza kwa asilimia 75.6 huku akifuatwa na mbunge wa Runyenjes Karemba Muchangi kwa asilimia 72.7.

Matokeo hayo ya hivi punde ya shirika la Leeway Africa, yamemuorodhesha Ndindi Nyoro wa Kiharu mbunge wa pili bor, akituzwa asilimia 70.2 huku Reuben Kiborek (Mogotio) akipata asilimia 70.1.

Mpuru Aburi ambaye ni mbunge wa Tigania Mashariki, ripoti ya utafiti huo imemtaja kuwa wa tano akizoa asilimia 69.8.

Matokeo ya utafiti wa shirika hilo yanakuja wiki moja baada ya Politrack Africa kuorodhesha matokeo yao ya wabunge 20 walio na utendakazi bora kwa miezi minane iliyopita.

Kwenye ripoti yao, Babu aliorodheshwa kama mbunge wa pili bora nchini akipewa asilimia 72.1.

Mbunge wa Kiharu, Ndindi Nyoro aliorodheshwa kidedea – bora zaidi kwa asilimia 73.7, huku Patrick Makau (Machakos) akiwa wa tatu (70.6).

  • Tags

You can share this post!

‘Ker’ mpya wa jamii ya Waluo kujulikana baada...

Mkongwe kutembea kilomita 300 kuadhimisha Madaraka Dei 2023...

T L