• Nairobi
  • Last Updated February 29th, 2024 6:55 PM
Huduma za M-Pesa kuzinduliwa nchini Ethiopia

Huduma za M-Pesa kuzinduliwa nchini Ethiopia

NA HELLEN GITHAIGA

BENKI ya Kitaifa ya Ethiopia imeikabidhi Safaricom leseni ya kuanzisha huduma za M-Pesa kuwapa raia wengi teknolojia rahisi ya kutuma na kupokea pesa.

Safaricom chini ya muungano wao wa ‘Consortium’ imesema itazindua huduma hizo nchini Ethiopia kabla ya mwisho wa mwaka huu 2023.

Huduma za M-Pesa zilizinduliwa rasmi nchini Kenya mwaka 2007.

“Safaricom Ethiopia imepata rasmi leseni ya kuzindua huduma za kutuma na kupokea pesa kwa simu. Tunatarajia kuzindua huduma za M-Pesa katika majuma yajayo,” Afisa Mkuu Mtendaji wa Safaricom Peter Ndegwa amesema Alhamisi akifikishia wawekezaji habari njema.

Muungano unaongozwa na Safaricom nchini humo ulilipa takriban Dola 150 milioni sawa na Sh18.9 bilioni kama ada ya leseni kwa Benki ya Kitaifa ya Ethiopia (NBE).

Muungano huo unaleta pamoja Safaricom, Vodacom Group Ltd (Afrika Kusini), Vodacom Group PLC (Uingereza), British International Investment Plc na shirika la Sumitomo.

  • Tags

You can share this post!

KINYUA KING’ORI: Serikali ikome kuongeza ushuru mpya...

Maaskofu wapata ujasiri kuikosoa serikali

T L