• Nairobi
  • Last Updated March 5th, 2024 5:55 AM
Israel yaanza tena kulipua Gaza muda wa kusitisha mapigano ukifika mwisho

Israel yaanza tena kulipua Gaza muda wa kusitisha mapigano ukifika mwisho

NA AFP

ISRAEL, JERUSALEM

JESHI la Israeli limeanza tena mapigano Gaza, huku mashambulizi ya anga na risasi yakiripotiwa katika mji wa Gaza.

Haya yanajiri wakati ambapo muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano hayo ukifika mwisho.

“Kundi la Hamas halikutii makubaliano yetu. Hii ndio maana vikosi vya Ulinzi vya Israeli vimeanza tena mapambano dhidi ya kundi hilo la kigaidi katika Ukanda wa Gaza,” jeshi la Israeli lilisema.

Tangazo hilo limejiri muda mfupi baada ya jeshi kusema kuwa limenasa roketi iliyorushwa kutoka Gaza, ikiwa ni ya kwanza kutoka eneo hilo tangu kombora liliporushwa dakika chache kabla ya siku ya kwanza ya kusitisha mapigano.

Ndani ya Gaza, mwandishi wa habari wa AFP alisema ndege za kivita za Israeli zilifanya mashambulizi, na kuripoti ufyatuaji wa mizinga katika mji wa Gaza.

Ndege zisizo na rubani pia ziliweza kusikika angani kusini mwa eneo hilo kwa mara ya kwanza tangu kusitishwa kwa makubaliano hayo, mwandishi wa AFP katika eneo hilo alisema.

Kuanza tena kwa mapigano kulikatisha matumaini ya kurefushwa kwa mapatano ya siku saba ambayo yamewafanya mateka kadhaa kuachiliwa huru.

Makubaliano hayo pia yaliruhusu msaada zaidi kuingia katika eneo lililoharibiwa la Ukanda wa Gaza.

Siku ya Alhamisi, mwanadiplomasia mkuu wa Amerika, Antony Blinken, alikutana na maafisa wa Israeli na Palestina, na kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano hayo kuongezwa.

Kando na hayo, alionya kuw ikiwa mapigano hayo yataanzishwa tena, basi raia wanafaa kulindwa.

Wakati wa mapatano yaliyosimamiwa na Qatar, mateka 80 wa Israeli waliachiliwa na pia wafungwa 240 wa Kipalestina.

Zaidi ya wageni 20, pia waliachiliwa.

Waisraeli sita zaidi, wengine wakiwa na uraia wa nchi mbili, waliachiliwa, saa chache baada ya wanawake wawili kuachiliwa.

Hilo lilifanya jumla ya walioachiliwa Alhamisi kufikia wanane, badala ya mateka 10 kwa siku.

Chanzo kilicho karibu na kundi hilo la wanamgambo kilisema kinawahesabu wanawake wawili wa Urusi-Israeli walioachiliwa Jumatano kama sehemu ya kundi la saba.

Kuachiliwa huko kulileta afueni kwa Keren Shem, ambaye binti yake Mia alikuwa miongoni mwa wale walioachiliwa.

Wakati uo huo, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alisema alimuagiza waziri wake wa mambo ya nje, Eli Cohen, kumwita balozi wa Uhispania ili kutoa karipio.

Hii ni kufuatia kauli ya aibu ya waziri mkuu wa Uhispania katika siku ambayo magaidi wa Hamas walipowauwa Waisraeli katika mji wa Jerusalem.

Wapiganaji wawili wa kundi la Hamas waliwaua raia watatu katika kituo cha mabasi cha Jerusalem asubuhi siku ya Alhamisi.

Kundi hilo la Palestina lina ngome yake katika Ukanda wa Gaza, ambako lilianzisha mashambulio ya Oktoba 7 nchini Israeli, na kusababisha vita.

  • Tags

You can share this post!

Msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed afungiwa nje ya kongamano...

Mhubiri Paul Mackenzie sasa asukumwa jela mwaka mzima

T L