• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 9:50 AM
Israeli na Hamas wabadilishana wafungwa na waliokuwa wametekwa

Israeli na Hamas wabadilishana wafungwa na waliokuwa wametekwa

NA MASHIRIKA

GAZA, Palestine

KUNDI la Hamas limeachilia mateka 24 waliokuwa wamezuiliwa Gaza kwa juma kadhaa na wafungwa 29 wa Kipalestina wakiachiliwa kutoka jela kwa awamu ya kwanza ya mabadilishano chini ya mpango wa kusitisha mapigano kwa siku nne.

Qatar ambayo ilikuwa mpatanishaji wa mpango wa kusitisha vita, ilisema tayari familia 13 za Israeli zimeachiliwa na Hamas na zimefarijika kurudi kwao.

Kundi hilo lililojumuisha watoto, wanawake na wanamme, walirejea nchini Israeli baada ya Shirika la msalaba kuwasaidia kuwatoa Gaza na kuwapeleka Misri.

Raia kumi wa Thailand na Mfilipino mmoja pia wameachilia, katika mkataba tofauti na ule uliopatanishwa na Qatar.

Mkataba huo ulikuwa na makubaliano ya jumla ya mateka Israeli 50 na wafungwa 150 wa Kipalestina ambao wanakusudiwa kuachiliwa kwa siku nne zijazo wakati wa kusitisha mapigano kwa muda.

Watu wa familia hizo 13 walipelekwa katika hospitali ya Misri ili kupata huduma za matibabu kabla ya kurudishwa Israeli.

Waisraeli hao, walikuwa watoto wanne wenye umri wa miaka 2, 4, 6 na tisa pamoja na bibi wa miaka 85.

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamini Netanyahu alisema wameweza kurejesha kundi la kwanza la wale waliokuwa wametekwa nyara.

“Nasisitiza kwenu, familia na raia wa Israeli tumejitolea kuwarudisha wote walitekwa nyara,” alisema Bw Netanyahu.

Miongo mwa walioachiliwa ni mke wa Yoni Asher Doron Katz Asher 34 na wanawe wawili.

Bw Asher aliambia BBC aliazimia kuangana na familia yake tena iliyokuwa imetekwa.

Aliongezea hatasherekea hadi wale wote waliotekwa nyara wamerejea nchini Israeli.

“Familia zilizotekwa si mabango, ni watu halisi. Familia za waliotekwa ni familia yangu mpya. Nitahakikisha nimefanya chochote kile kuhakikisha wamerejea nyumbani,” alisema Bw Asher.

Pia, familia za raia wa Thailand na Filipino wanayonafuu baada ya Hama kuwaachilia.

Kittiya Thuengsaeng aliambia maafisa wa Thai kuwa mpenzi wake wa miaka 3 aliaga kwenye mapigano hayo ila maafisa hao wakatangaza maajina ya waliouliwa na jina la mpenziwe halikuwepo.

Siku tano alipokea taarifa yupo miongoni mwa wale waliokuwa wametekwa nyara.

Wafungwa 39 wakipalestina waliachiliwa baada ya kutumika kwenye mabadilishano kwenye mkataba uliokuwa umewekwa.

Watuhumiwa hao, walishtakiwa na makosa mbalimbali kama vile kurusha mawe na kujaribu kuua. Wengine wakihukumiwa kwa uhalifu baadhi yao wakisubiri kesi za kusikillzwa.

Wafungwa hao walichanguliwa kutoka kwenye orodha ya wanawake na watoto 300 waliokuwa wamekamatwa na Israeli.

Robo ya orodha hiyo wengi wamehukumiwa na kuzuiliwa rumande huku wakisubiri kesi zao kusikilizwa.

Asilimia 40 ikiwa ni wavulana matinées chini ya miaka 18.

Hamas waliwateka watu zaidi ya 200 wakati wa kuvuka mpaka wa Kusini Israeli Oktoba 7 na kuwaua watu 1200.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema idadi ya wapalestina waliotiwa baroni bila kufunguliwa mashtaka katika jela za Israeli imeongezeka tangu shambulizi hilo.

Takribani malori 60 ya misaada imefika Gaza na manne nchini Israeli ikiwa na mafuta lita 130,000 baada ya mapigano hayo kusitoshwa.

  • Tags

You can share this post!

Baba wa watoto 16 Mandera ashangaza wengi kwa kujizolea...

KNEC yakiri kulikuwa na dosari katika matokeo ya KCPE

T L