• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 1:29 PM
Maajabu mwanamke Afrika Kusini akivunja rekodi ya dunia kujifungua watoto 10

Maajabu mwanamke Afrika Kusini akivunja rekodi ya dunia kujifungua watoto 10

Na SAMMY WAWERU

MWANAMKE mmoja nchini Afrika Kusini alivunja rekodi ya dunia Jumatatu kwa kujifungua watoto 10, taji lililokuwa limeshikiliwa na Malian Halima Cissé, wa Morocco aliyejifungua watoto tisa mwezi uliopita.

Gosiame Thamara Sithole, alipata watoto hao na ambao hawakuwa wamefikisha umri wa kuzaliwa, katika hospitali moja mjini Pretoria.

“Ni wavulana saba na wasichana watatu. Wakati wa kujifungua alikuwa na ujauzito wa miezi saba na siku saba. Nina furaha. Nina hisia za kutuliza moyo. Sitaongea mengi. Tutazungumza mengi baadaye,” mume wake Teboho Tsotetsi akaambia shirika la habari la Pretoria News.

Mama huyo mwenye umri wa miaka 37 alisema alishangazwa na ujauzito wake.Hata hivyo anasema alikuwa na shauku awali madaktari walipomueleza ana ujauzito wa watoto wanane.Hadi kujifungua kwake, alidhania ni watoto wanane.

“Sikuamini. Nilikuwa na shauku. Nilidhania wangekuwa mapacha au watoto watatu, na si zaidi ya hao. Daktari aliponieleza sikuamini, ilinichukua muda.“Hata nilipoonyeshwa picha, sikuamini. Muda ulivyozidi kusonga, niliitikia. Ingawa nilikuwa na ugumu wa kulala usiku,” akasema Tsotetsi na ambaye hana kazi.Alisema alijiona yeye ni kati ya watoto wa Mungu waliojaaliawa.

“Ni baraka kujaaliwa idadi ya watoto kama hawa. Wengi kule nje hawana watoto, ni baraka ninazoridhia. Nililazimika kufanya utafiti wangu binafsi kubaini ikiwa mtu anaweza kujifungua watoto wanane. Lilikuwa jambo geni. Nilifahamu kuhusu mapacha, watoto watatu au wanne pekee,” akasimulia.

Alisema Sithole, na ambaye ni meneja wa duka moja la bidhaa rejareja alikuwa na ujauzito uliompa nyakati ngumu, akihisi maumivu ya mara kwa mara ya miguu na kiungulia.

Profesa Dini Mawela, naibu mkuu wa masuala ya matibabu Chuo Kikuu cha Sefako (kinachohusiana na masuala ya matibabu), alisema suala la Sithole ni la kipekee.

  • Tags

You can share this post!

Giroud na Griezmann wasaidia Ufaransa kuzamisha Bulgaria

Bondia Okwiri kupigania mamilioni Agosti, Mike Tyson...