• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 8:55 AM
Mashambulio makali nchini Sudan mahitaji ya chakula yakiongezeka

Mashambulio makali nchini Sudan mahitaji ya chakula yakiongezeka

NA MASHIRIKA

KHARTOUM, SUDAN

MASHAMBULIO makali ya anga yametokea maeneo ya kusini mwa jiji kuu la Sudan, Alhamisi huku mapigano yakipamba moto karibu na kambi ya kijeshi.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, mapingano hayo yamesababisha zaidi ya watu milioni moja kutoroka makwao na kuwaacha wakaazi wa Khartoum wakihangaika.

Mashambulio ya anga ya jeshi yanayolenga kikosi cha Rapid Special Forces (RSF) yalisikika katika vitongoji kadhaa vya makazi kusini mwa Khartoum.

Zaidi ya hayo, eneo lingine lililolengwa ni pamoja na karibu na kambi ya Taiba, wakati kikosi cha polisi cha akiba kilichoshirikiana na jeshi kikipambana na RSF uwanjani, mashahidi walisema.

Baada ya maapigano kuzuka tena mnamo Jumatatau wiki hii, Jeshi limetumia zaidi nguvu za anga na silaha nzito wakati likijaribu kuwarudisha nyuma RSF.

Kundi la RSF ambayo lilikuwa lemeenea katika maeneo makubwa ya Khartoum na miji inayopakana nayo ya Bahri na Omdurman katika mto Nile baada ya mapigano kuzuka Aprili 15.

“Mashambulio ya mabomu na mapigano hayakomi na hakuna njia ya kutoroka kutoka kwa nyumba zetu. Pesa zetu zote zimeishwa,” Bw Salah el-Din Othman, mkaazi wa Khartoum mwenye umri wa miaka 35 akasema.

Bw Othman aliongeza kwamba licha ya watu kutaka watoroke makwao, wenyeji wanahofia magenge ya waporaji watapora mali kutoka kwa nyumba zao.

“Hata kama tutafanikiwa kutoka nje ya nyumba zetu, tunaogopa kwamba magenge yatapora kila kitu ndani ya nyumba … tunaishi katika jinamizi la woga na umaskini.”

Isitoshe, ghasia pia zimepamba moto eneo la Darfur magharibi mwa Sudan na katika Jimbo la Kordofan Kaskazini, na maeneo mengine ya nchi, lakini mzozo wa madaraka umekuwa ukilenga mji mkuu.

Mkuu wa jeshi, Abdel Fattah al-Burhan na kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana kama Hemedti, wanakisiwa kusalia Khartoum wakati wote wa mapigano.

Mnamo Jumatatu wiki hii, jeshi lilitoa mkanda wa video ukimuonyesha Burhan akiwa amevalia magwanda ya kivita ya jeshi akisalimiana na wanajeshi katika kile kilichoonekana kuwa makao makuu ya jeshi katikati mwa jiji la Khartoum.

Kadhalika, kulingana na makadirio ya hivi punde, zaidi ya watu 840,000 wwametoroka makwao nchini Sudan huku watu wengine zaidi ya 220,000 wakiripotiwa kutorokea nchi jirani.

a Hemedti, wanakisiwa kusalia Khartoum wakati wote wa mapigano.

Mnamo Jumatatu wiki hii, jeshi lilitoa mkanda wa video ukimuonyesha Burhan akiwa amevalia magwanda ya kivita ya jeshi akisalimiana na wanajeshi katika kile kilichoonekana kuwa makao makuu ya jeshi katikati mwa jiji la Khartoum.

Kadhalika, kulingana na makadirio ya hivi punde, zaidi ya watu 840,000 wametoroka makwao nchini Sudan huku watu wengine zaidi ya 220,000 wakiripotiwa kutorokea nchi jirani.

Mpango wa Chakula Duniani (WFP) umesema timu yake iko kwa majimbo sita nchini Sudan ikilenga kusaidia watu 4.9 milioni walio katika hatari kubwa ya kukosa chakula, pamoja na wale wanaotorokea nchi jirani za Chad, Misri na Sudan Kusini.

  • Tags

You can share this post!

Mlanguzi sugu wa dawa za kulevya aliyelemea askari

DPP Haji apinga kufunguliwa kwa akaunti 30 za Pasta Odero,...

T L