• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 2:11 PM
Mpinzani jela miaka 7 kwa ‘kumtusi’ Rais Tshisekedi

Mpinzani jela miaka 7 kwa ‘kumtusi’ Rais Tshisekedi

NA MASHIRIKA

KINSHASA, DRC

MAKAHAMA Kuu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imemhukumu mgombea urais Jean-Marc Kabund kifungo cha miaka saba jela kwa makosa 12 likiwemo kumtusi Rais Felix Tshisekedi.

Mbali na hayo, wakili wake Kabund alisema kosa lingine dhidi ya mteja wake lilikuwa kueneza uvumi na uzushi.

Kabund alikuwa makamu wa rais wa zamani wa bunge na mshirika wa karibu wa Rais Felix Tshisekedi ambaye alizindua chama chake cha kisiasa mwaka jana baada ya wawili hao kutofautiana.

Amekuwa akizuiliwa katika gereza kuu la Kinshasa tangu kukamatwa kwake Agosti 2022, baada ya kumuita Tshisekedi “hatari” na kuikashifu serikali yake katika hotuba.

“Mahakama ilimhukumu kifungo cha miezi minne kila mmoja kwa makosa tisa ya kwanza na miezi 16 kila moja kwa makosa matatu ya mwisho,” wakili wa Kabund, Kadi Diko aliambia shirika la Reuters.

Aliongeza kuwa makosa makubwa zaidi ni “kueneza uvumi wa uongo” na “kumdharau rais” na “bunge”.

Wakili Diko alisema maamuzi ya mahakama yalikuwa makali sana akidai haukuruhusiwa kukata rufaa.

“Nimewaomba wananchi kufanya kila wawezalo kuhakikisha Tshisekedi anaondolewa katika uchaguzi ujao, kwa sababu ninaamini nchi iko katika hatari kubwa chini ya uongozi wake,” aliambia korti mnamo Agosti.

DRC inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu mnamo Desemba 20 ambapo Tshisekedi huenda akawania muhula wa pili.

Tofauti za kisiasa zimekuwa zikiongezeka kabla ya siku ya kupiga kura.

Mwezi Julai, Msemaji wa upinzani aliuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa wakiandamana kupinga ukiukwaji wa taratibu katika usajili wa wapiga kura.

Kabund alihukumiwa na Mahakama ya Cassation, mojawapo ya mahakama kuu nchini Congo, ambayo hairuhusu walalamishi kukata rufaa.

  • Tags

You can share this post!

Kindiki awafokea wanasiasa wanaohujumu juhudi za amani,...

Kemsa kuteketeza dawa za Sh1.8 bilioni zilizoharibika

T L