• Nairobi
  • Last Updated October 2nd, 2023 11:00 AM
Rais Museveni: Ambukizo la corona limesababisha likizo ya lazima katika miaka 53 ya utendakazi wangu

Rais Museveni: Ambukizo la corona limesababisha likizo ya lazima katika miaka 53 ya utendakazi wangu

NA SAMMY WAWERU

RAIS wa Uganda Yoweri Museveni ametaja ambukizo la corona la hivi punde, kama shinikizo la likizo ya pili ya lazima katika kipindi cha miaka 53 ya utendakazi wake.

Alhamisi, Juni 8, 2023, akitoa taarifa kuthibitisha kuugua Homa ya Corona, Bw Museveni alifichua kwamba likizo ya kwanza ya lazima ilikuwa mwaka wa 1971.

“Corona niliyopata, imelazimisha likizo ya pili katika utendakazi wangu tangu miaka 53 iliyopita tulipoanza ‘kupigana’ na Idi Amin,” Rais huyo wa nchi jirani alielezea kupitia taarifa kwenye akaunti yake ya Twitter.

Marehemu Idi Amin alikuwa Rais wa tatu wa Uganda, aliyetawala taifa hilo kati ya 1971 – 1979.

Rais Museveni alitwaa mamlaka 1986.

Akisisitiza kuwa makini dhidi ya Covid-19, Museveni alisema alilazimika majuzi kuacha kuvalia barakoa – maski kutokana na athari za mzio (allergy) machoni na kooni.

“Mnakumbuka nilipopoteza sauti mara mbili wakati wa uchaguzi? Ni kwa sababu ya mzio.”

Rais Museveni alisema alianza kushuhudia dalili za Homa ya Corona Jumanne, Juni 6, 2023.

  • Tags

You can share this post!

Wahudumu wawili wa bodaboda wafariki baada ya kugongwa na...

Museveni achapa kazi licha ya kupimwa na kupatikana ana...

T L