• Nairobi
  • Last Updated December 8th, 2023 10:25 PM
Watu 6,000 waangamia baada ya kimbunga kupiga eneo la kaskazini mashariki mwa Libya

Watu 6,000 waangamia baada ya kimbunga kupiga eneo la kaskazini mashariki mwa Libya

Kulingana na ripoti iliyotolewa na maafisa wa serikali katika eneo la Derna mnamo Jumatano, jumla ya watu 6,000 walikuwa wamethibitishwa kufariki katika mkasa uliokumba mji huo ulioko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

“Idadi ya waliokufa inatarajiwa kuongeza huku shughuli za uokoaji zikiendelea katika mji wa Derna ulioko karibu za bahari ya Mediterrennean. Magari ya makundi ya uokoaji na yale ya kupeleka misaada yanajaribu kufika mji huo kwa kupitia barabara moja pekee inayotumika wakati huu,” taarifa kutoka Wizara ya Masuala ya Ndani.

Nayo Wizara ya Afya ilisema kuwa zaidi ya miili 1,000 imetolewa katika vijiji na makazi yaliyofunikwa na mafuriko hayo yaliyosababishwa na kimbunga Daniel mnamo Jumatatu.

“Miili mingine karibu 700 imezikwa,” akasema Waziri wa Afya Othman Abduljalil.

Mabwawa mawili pia yaliporomoka katika mkasa huo ambao ulisababishwa na mvua kubwa zaidi iliyoshuhudiwa katika mji wa Derna na maeneo ya karibu.

“Maelfu ya wakazi bado haijulikani waliko katika miji minne ya mashariki mwa Libya. Hii ni kwa sababu makazi mengi yako karibu na mikondo ya maji,” wakasema maafisa wa shirika la International Federation of Red Cross na lile la Red Crescent.

Miundo msingi nchini Libya imetelekezwa kutokana na misukosuko ya kisiasa ya muda mrefu.

Hii ndio maana barabara na nyaya za umeme na zile za mawasiliano zimeharibiwa na mafuriko hayo, hali inayohujumu shughuli za uokoaji. Ubovu wa miundo msingi pia umeongeza hofu kuhusu kuongezeka zaidi kwa idadi ya waliokufa.

Waziri Abduljalil alibashiri kuwa huenda kuna miili mingi ambayo bado imekwama ndani ya majengo yaliyoathirika na maji ya mafuriko katika mji wa Derna na maeneo yaliyo karibu.

“Kuna familia bado zimekwama ndani ya nyumba zao na kuna waathiriwa chini ya mabaki ya nyumba. Pia kuna uwezekano mkubwa sana kuwa wengine wamesombwa na maji baharini. Shughuli za kuwatafuta wengine ambao huenda waliangamia katika janga hilo zinaendelea,” akaongeza.

Wataalamu wanasema kimbunga hicho ni matokeo ya shinikizo la chini lililosababisha mafuriko makubwa nchini Ugiriki wiki iliyopita na kisha kuipiga Bahari ya Mediterrenean kabla ya kuzuka kwa kimbunga kingine kinachojulikana kama “medicane”.

Hapo awali, Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Libya lilikadiria kuwa zaidi ya watu 2,900 walikufa eneo la Derna, kulingana na taarifa yake kwenye mtandao wa kijamii.

Naye msemaji wa Jeshi la Kitaifa la Libya (LNA) lenye makao yake mashariki mwa Libya, Ahmed Mismari, alithibitisha kuporomoka kwa mabwawa mawili kutokana na mafuriko hayo.

“Aidha madaraja matatu yaliporomoka. Hii iliathiri shughuli za uchukuzi kuingia na kutoka maeneo yaliyo karibu na madaraja hayo,” akasema Mismari.

Mkuu wa mamlaka ya Dharura na Ambulensi nchini humo, Osama Aly, alisema kwamba baada ya bwawa hilo kuporomoka, maji yote yalielekea eneo la Derna.

Nyumba zilizo kwenye mabonde na magari zilisombwa.

“Hali ya anga haikuchunguzwa vizuri, viwango vya maji baharini na mvua na kasi ya upepo haikuchunguzwa vizuri. Kadhalika, wananchi wahakuhamasishwa kuhusu athari za janga kama hilo,” akasema Aly.

  • Tags

You can share this post!

Maguire alivyofanya ‘ile kitu’ mara hii kwa...

Demu alia kukosa ‘nyota’ ya kupata dume la...

T L