Kimataifa

Habibu alinitema baada ya kuugua, alia mwanamitindo

January 23rd, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWANAMKE mmoja aliyekuwa mwanamitindo na ambaye sasa anaugua ugonjwa wa akili amemlaumu aliyekuwa mpenzi wake kuwa alimtema siku chache kabla yao kufunga ndoa, wakati aliugua na kulazwa hospitalini.

Bi Emily Nicholson, 24, alisema kuwa walikuwa wameelewana na mpenzi wake Jamie Smith, lakini baadaye akabainika kuwa na ugonjwa wa uvimbe kwenye akili na kuambiwa kuwa alikuwa na mwaka mmoja tu wa kuishi.

Emily alisema kuwa wiki moja kabla ya harusi yao, mpenzi wake Jamie aliamua kumtema, kupitia ujumbe wa ‘Messenger’ kwenye Facebook.

Mwanamke huyo aidha alihofia kuwa sababu ya mpenzi wake kumtema ilikuwa dawa alizokuwa akitumia alipougua, ambazo zilimfanya kunenepa kupita kiasi.

Emily alieleza mashirika kuwa “Janie alisema kuwa hakutaka kuwa name na kuwa hakuwa akinipenda kwa muda mrefu.”

“Kwa miezi mingi alikuwa akienda kujiburudisha na marafiki zake lakinimimi singefanya hivyo kwa kuwa nilikuwa mgonjwa.

“Kwa sasa simpendi tena kwa kuwa alinichoma rohoni lakini sina sababu ya kukasirika.”

Wapenzi hao wawili walipatana walipokuwa Australia.

Japo madaktari walimpa mwaka kuishi, alipiku matarajio yao na sasa madaktari wanasema kuwa amepitisha muda wa kuishi.

Sasa alihama kuishi Uingereza na familia yake inajikaza kuchanga Zaidi ya Sh4milioni ili atibiwe.

Lakini kwa upande wake, Janie anapinga kuwa alimtema Emily, akisema “haikuhusiana vyovyote na kunenepa.”