Habari

Hafla ya kumuenzi Mzee Maulidi Juma yafana mjini Mombasa

February 15th, 2020 1 min read

Na HASSAN MUCHAI

HAFLA ya kumuenzi Mzee Maulidi Juma imefana mjini Mombasa mnamo Jumamosi.

Wadau kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamejumuika katika ukumbi wa RISSEA mjini Mombasa kumuenzi mzee huyo kikosi cha ‘Taifa Leo’  kikiwa mstari wa mbele huku navyo vyombo vingine vya habari vikivutiwa.

Gazeti la ‘Taifa Leo’ kupitia chama cha WAKITA limewakilishwa na mwenyekiti Abdul Noor pamoja Naibu wake Bw Kinyua Kingori.

Wengine wamekuwa Hassan Morowa, Wanto Warui, mwandishi habari Mishi Gongo, Salim Makayamba miongoni mwa wengine.

Baadhi ya waandishi wa habari waliofika ukumbi wa RISSEA mjini Mombasa kumhoji Maulidi Juma. Picha/ Hassan Muchai
Mzee Maulidi Juma (wa pili kulia kwa walioketi) baada ya kuenziwa kwa mavazi rasmi ya Kigiriama Februari 15, 2020, katika ukumbi wa RISSEA mjini Mombasa. Picha/ Hassan Muchai
Mzee Maulidi Juma baada ya kuenziwa kwa mavazi rasmi ya Kigiriama katika ukumbi wa RISSEA mjini Mombasa Februari 15, 2020. Picha/ Hassan Muchai
Bi Zulfa Mohammed kutoka Mombasa ni miongoni mwa waliofika katika ukumbi wa RISSEA mjini Mombasa Februari 15, 2020, kumuenzi Mzee Maulidi Juma. Picha/ Hassan Muchai
Amekuwepo pia Ustadh Wallah Bin Wallah. Picha/ Hassan Muchai
Mwenyekiti wa Wakita Bw Abdul Noor. Picha/ Hassan Muchai
Bi Amira Mselem kutoka kituo cha RISSEA akihutubia hadhira. Picha/ Hassan Muchai