Haji aamuru polisi sita washtakiwe kwa mauaji ya ndugu wawili

Haji aamuru polisi sita washtakiwe kwa mauaji ya ndugu wawili

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI wa mashtaka ya Umma Noordin Haji Jumatatu aliagiza kukamatwa kwa maafisa sita wa polisi kuhusiana na mauaji ya kaka wawili eneo la Kianjokoma kaunti ya Embu.

Maafisa hao wanahudumu katika kituo cha polisi cha Manyatta.Bw Haji alisema kwa kuwa  mauaji hayo yalitendeka kaka hao wakiwa mikononi mwao ni lazima ukweli ujulikane.

“Nimeagiza niletewe faili punde uchunguzi wa mamlaka ya uchunguzi wa utenda kazi wa polisi IPOA utakapokamilika, lakini ripoti za awali zinanilazimu nimwamuru Inspekta Jenerali wa Polisi akamate maafisa waliohusika na wafikishwe kortini Nairobi,” alisema Bw Haji.

Benson Njiru Ndwiga na Emmanuel Matura Ndwiga waliuawa usiku wa Agosti 1, 2021 baada ya kukamatwa na Polisi kwa madai ya kukiuka saa za Kafiu.Njiru na Matura walitoweka baada ya kufungaMaafisa sita ni Koplo wawili na Konstebo wanne.

Maafisa wahusika walidai ndugu hao waliruka kutoka gari la polisi kwenye barabara ya Kiriare-Buvori na iliguduliwa hawakuwa garini ilipofika stesheni.

  • Tags

You can share this post!

AKILIMALI: Avuna hela kutokana na ufugaji sungura na njiwa...

Mahabusu alalama Kortini hakupewa chakula akiwa rumande