Haji amwamuru Boinnet achunguze ajali ya Fort Ternan

Haji amwamuru Boinnet achunguze ajali ya Fort Ternan

Na CHARLES WASONGA

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) Nordin Haji amemtaka Inspekta Jenerali wa polisi Joseph Boinnet kuwachunguza maafisa wa serikali ambao walichangia kutokea kwa ajali mbaya ya iliyotokea Kericho kwa kuzembea kazini.

Bw Haji ametoa agizo hilo siku moja baada ya basi kwa jina Home Boyz kuhusika katika ajali katika eneo la Fort Ternan katika barabara la Londiani- Muhoroni na kupelekea kuuawa kwa watu 58.

Ajali hiyo ilitoa Jumatano alfajiri basi hilo ambalo lilijaaa abiri na mizigo kupita kiasi lilipokuwa likisafiri kutoka Nairobi kwenda Kakamega. Abiria wengine 15 walijeruhiwa vibay sana na wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kericho huku madai yakiibuliwa kwamba basi hilo lilikiuka sheria za trafiki.

Kwenye barua ambayo nakala zake zilitumwa kwa vyombo vya habari Alhamisi jioni Bw Haji pia alimtaka Bw Boinnet kuchunguza asasi zote za serikali zilizopewa jukumu la kudumisha usalama barabarani nchini.

Barua hiyo ya Haji inasema: “Nakuamuru kwamba uchunguze kuhusu suala hili ufanyike kubaini watu ambao huenda, kwa kutowajibika, walichangia kwa njia moja ama nyingine, katika ajali iliyosababisha mauaji katika Fort Tenan, kaunti ya Kericho”.

Anaendelea kusema: “Baada ya uchunguzi kukamilika utuwasilishie faili ili tutoa mwelekeo ufaao.”

Amri ya Bw Haji inajiri saa chache baada ya Bw Boinnet kuamuru kwamba maafisa wa polisi waliokuwa wakisimamia ruti ya Londiani- Muhoroni wachunguwe.

Akasema: “Ni wajibu wa makamanda wa kaunti kudhibiti na kuhakikisha sheria za trafiki zinazingatiwa. Na ikiwa itabaini kuwa kamanda wa polisi katika kaunti ya Kericho alizembea kazini ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria,” akasema Bw Boinnet alipowahutubia wanahabari katika Makao Makuu ya Hamlaka ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) Nairobi.

“Vile vile, tunashauriana ili kuwatambua maafisa wa polisi ambao walikuwa katika vizuizi mbalimbali na ikiwa waliruhusu basi hilo kuendelea na safari licha ya kuvunja sheria za trafiki,” akaongeza.

You can share this post!

Wabunge na maseneta wamtaka Uhuru kumwadhibu Boinnet kuhusu...

Waziri Mkuu awafanyisha wanajeshi mazoezi kuzima maandamano

adminleo