Habari za Kitaifa

Hakuna stima kote nchini, Wizara ya Kawi yathibitisha

May 2nd, 2024 1 min read

Na MWANDISHI WETU

WIZARA ya Kawi na Petroli imethibitisha kupotea kwa nguvu za umeme kote nchini kuanzia saa kumi na moja unusu Alhamisi, Mei 2, 2024.

Kulingana na taarifa fupi kwa wanahabari, wizara inasema kwamba kumetokea tatizo kati ya Kamburu na Dandora na kwamba kila juhudi zinafanywa kurekebisha hali.

“Mnara umekumbwa na changamoto zinazotokana na mafuriko ambayo yamegubika nchi. Lakini stima zitarejea hivi karibuni katika muda wa saa mbili,” ikasema taarifa hiyo.

Mengi zaidi ni kadiri tunavyoyapokea….