Habari Mseto

Hali ngumu ya uchumi yapunguza faida ya benki ya Co-operative

March 20th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Benki ya Co-operative imeandikisha kupungukiwa kwa faida baada ya mapato yake kutozwa ushuru kwa mwaka wa 2017.

Mapato yake yalipungua kwa asilimia kwa asilimia 10.24. Ilipata faida ya Sh11.4 bilioni ikilinganishwa na Sh12.7 bilioni kipindi hicho mwaka wa 2016.

Upungufu wa mapato yake ulitokana na kudhibitiwa kwa viwango vya riba na Benki Kuu, ilisema benki hiyo Ijumaa.

Lakini pia, hali hiyo ilisababishwa na hali ngumu ya kibiashara na uchumi. Mapato kutokana na rehani za serikali yalipungua kwa asilimia tatu hadi Sh8.2 bilioni ilhali mapato kutokana na mikopo yalipungua kwa asilimia 4.7, alisema meneja mkurugenzi Gideon Muriuki.

Licha ya upungufu huo, benki hiyo ilisema hali haikuwa mbaya sana, hasa kutokana na kubuni mikakati ya kukabiliana na hali kama hizo hasa katika kupunguza gharama ya operesheni na jinsi ya utoaji wa huduma kwa wateja, kama vile ‘Soaring Eagle.’