Hamna jingine bali kunichagua mimi, Trump ajipiga kifua

Hamna jingine bali kunichagua mimi, Trump ajipiga kifua

Na MASHIRIKA na MARY WANGARI

mwnyambura@ke.nationmedia.com

RAIS Donald Trump amegonga vichwa vya vyombo vya habari baada ya kuwadhalilisha vibaya washindani wake watarajiwa katika uchaguzi wa 2020 na kujipiga kifua kwamba ndiye anayefaa zaidi kwa uchumi wa Amerika.

Trump alizungumza kwa muda karibia saa moja na nusu mnamo Alhamisi, Agosti 15, 2019, katika mkutano wa kampeni mjini New Hampshire, ambapo aliwaponda wapinzani wake wa Democrats, na kudai taifa la Amerika halikuwa na hiari ila kumchagua, kwa kuwa yeye ndiye chaguo bora zaidi.

“Iwapo kwa sababu fulani singeshinda uchaguzi, masoko haya yangekuwa yameporomoka, na hilo litatendeka hata zaidi 2020. Hivyo basi haijalishi iwapo mnanipenda au mnanichukia, ni lazima mtanichagua,” alisema Rais huyo.

Alichambua orodha ya wagombea wakiwemo Elizabeth Warren na Kamala Harris, aliyekuwa mwakilishi Beto O’Rourke na aliyekuwa Naibu Rais Joe Biden, alihakikisha wameonja makali ya dhihaka zake.

“Je, vipi kuhusu mkutano wa kuchusha wa Joe Biden? Sivyo? Hakika amejishindia katika baadhi ya visa,” alisema Rais huyo akirejelea visanga vya kufedhesha vya naibu rais huyo wa zamani.

Akaongeza: “Kwa namna fulani natumai ni yeye.”

You can share this post!

Muumini apokonya kanisa viti

Ulinzi yatoka sare na Uganda

adminleo