Michezo

Harambee Stars yapokea mavazi rasmi ya kutumika Afcon

June 15th, 2019 1 min read

Na JOHN ASHIHUNDU

PARIS, Ufaransa

MAVAZI rasmi yatakayotumiwa na kikosi cha Harambee Stars wakati wa michuano ya AFCON yamepokelewa kwenye kambi ya kikosi hicho nchini Ufaransa.

Harambee Stars inakutana na DR Congo katika mechi ya kupimana nguvu Jumamosi siku, itaondoka eneo la Marcoussis nchini Ufaransa Jumatano kuelekea Misri kwa kipute hicho cha siku 28.

Kikosi hicho cha kocha Sebastien Migne kitatumia mavazi ya Macron ambayo waliyatumia kwa mara ya kwanza kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Madagascar ambapo walishinda 1-0.

Rais wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF), Nick Mwendwa alisema mavazi hayo yanatarajiwa kufika Nairobi kesho Jumatatu kwa mashabiki watakaotaka kuyanunua.

Harambee Stars ina mkataba wa miaka mitatu na kampuni ya Macron ambayo itatoa mavazi kwa timu hiyo ya taifa kwa kipindi hicho.