Hasira polisi aliyehusishwa na ubakaji akitoweka

Hasira polisi aliyehusishwa na ubakaji akitoweka

NA MAUREEN ONGALA

VIONGOZI katika Kaunti ya Kilifi, wameghadhabishwa baada ya idara ya usalama kudai haijui aliko afisa wa polisi alyehusishwa na ubakaji katika kaunti hiyo.

Polisi wa kituo cha Marereni, eneobunge la Magarini, alikuwa amedaiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15 mnamo Novemba 5.

Naibu Kamanda wa Polisi wa Kilifi, Bw Willy Simba, alidai kuwa mshukiwa alitoweka alipotambua kwamba kuna mipango ya kumkamata.

“Haiwezekani kwamba kuna rasilimali za kutosha wakati polisi wanataka kukamata wanawake wanaouza mnazi, ilhali wanashindwa kumkamata mwenzao aliyenajisi mtoto. Tutawapa magari pamoja na mafuta ili waende wamkamate mshukiwa huyo,” akasema Gavana wa Kilifi, Bw Gideon Mung’aro.

Mbunge Mwakilishi wa Kilifi, Bi Getrude Mbeyu, na Waziri wa Utumishi wa Umma na Jinsia, Bi Aisha Jumwa, walisema msimamo huo wa Bw Simba ni mzaha.

You can share this post!

DRC kuandaa uchaguzi mkuu mzozo ukichacha

Ruto afuata nyayo za Moi katika kutawala

T L