Habari Mseto

Hatimaye jumwa ajiwasilisha kwa polisi

August 30th, 2020 1 min read

Na Mohamed Ahmed

Baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji kuagiza kukamatwa kwa Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa na wengine ambao wanahusika na kesi ya wizi wa pesa Sh57 milioni, wapelezi wameanza kuwatafuta maramoja.

Bi Jumwa alienda mafichoni kuanzia Alhamisi hadi Jumapili alipotokea nyumbani kwake Nyali na kwenda kurekodi taarifa katika kituo cha polisi.

“Sasa naelekea kituo cha polisi cha Bandarini. Nimesikia fununu kwamba nimekamatwa. Sijakamtwa najipeleka kwenye kituo cha polisi kuandikisha taarifa,” aliambia mwanahabari kwenye mahojiano mafupi kabla ya kuingia kwa gari.

Hakimu mkuu wa Mombasa Edna Nyaloti aliangiza mbunge huyo ajiwasilishe kwa polisi kabla ya kufika kortini Jumatatu.

Hata hivyo Bi Jumwa alisema kwamba hakuwa na habari kwamba polisi walikuwa wanamtafuta.

“Niko hapa kwasababu korti iliniagiza nifika hapa. Nilikuwa Nairobi. Sijui ni kosa gani limefanya nikamatwe lakini nitawasikiza kesho kortini,” alisema.

Waliokamatwa mapema  ni Wachu  Omar meneja wa pesa za CDF , Sophia Said, Bernard Riba, Margaret Faith Kalume na Robert Katana na mhandisi wa serikali Kennedy Otieno Onyango.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA