Hatimaye mitihani yaanza kwa KCPE

Hatimaye mitihani yaanza kwa KCPE

Na CHARLES WASONGA

WAZIRI wa Elimu, Prof George Magoha amewahakikishia watahiniwa na wazazi kwamba mikakati imewekwa kulinda karatasi za mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) unaoanza leo saa mbili asubuhi.

Jumla ya wanafunzi 1,191, 725 wanafanya mtihani huo katika vituo 28, 467 kote nchini katika mazingira ya kipekee ya uzingativu wa masharti ya kuzuia msambao wa Covid-19 ulio katika wimbi lake la tatu. Jumla ya walimu 227,679 watasimamia mtihani huo na ule wa kidato cha nne (KCSE) unaoanza Machi 26, 2020.

Kwenye taarifa, Prof Magoha alisema usalama utaimarishwa katika vituo vyote vya mitihani kuhakikisha kuwa jaribio lolote la wizi wa mtihani linazimwa.

“Karatasi zote za mitihani ya KCPE na KCSE ziko salama na hazijaonwa na mtu yeyote kinyume cha sheria. Nawataka watahiniwa na wazazi wote kuwa watulivu kwani mtihani wa KCPE utaanza Jumatatu (leo) ilivyoratibiwa,” akaeleza kupitia akaunti ya Twitter ya Wizara ya Elimu.

Prof Magoha vile vile alipuuzilia mbali madai yaliyokuwa yakisambaa Jumamosi kwamba ndege iliyoanguka katika Kaunti ya Marsabit ilikuwa imebeba karatasi za mitihani ya KCPE.

“Hayo ni madai ya uwongo na yanayolenga kuwatia wasiwasi watahiniwa na wazazi bila sababu zozote. Ndege haikuwa imekodiwa na Wizara ya Elimu kwa shughuli zozote zinazohusiana na mitihani. Karatasi za mitihani ya kitaifa ziko salama,” akakariri.

Mitihani ya kitaifa ya mwaka huu ni ya aina yake kwani imefanyika miezi mitano kuchelewa kutokana na mlipuko wa janga la Covid-19 uliosababisha shule zote kufungwa kwa miezi tisa kuanzia Machi 15, 2020.

Mitihani hiyo ilikuwa imepangiwa kufanyika kuanzia Oktoba 27, 2020 lakini ikaahirishwa kutokana na changamoto hiyo ya kiafya iliyopelekea kutayarishwa upya kwa kalenda ya masomo. Chini ya kalenda hiyo mpya, wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha nne walirejelea masomo yao Oktoba 12, 2020. Wanafunzi wa gredi ya nne pia walifungua shule wakati huo.

Watahiniwa wa KCPE waliandikisha matokeo mabaya katika mtihani wa majaribio waliofanya Januari mwaka huu, hali iliyosababisha wadau kuingiwa na hofu kwamba huenda hali itakuwa hivyo katika matokeo ya mtihani unaoanza leo.

Hata hivyo, Profesa Magoha alipuuzilia mbali dhana akisema matokeo ya mtihani huo hayakupaswa kutumiwa kukadiria matokeo halisi katika KCPE.

“Matokeo haya hayaakisi uwezo kwa sababu waliufanya wiki chache baada ya kurejelea masomoni. Nina uhakikisha kuwa watoto wetu watafanya vizuri katika mitahi ujao wa KCPE. Walimu wetu wamekuwa wakifanya kazi nzuri ya kuwaandaa,” akasema wakati huo akielezea matumaini kuwa watahiniwa wataandisha matokeo mazuri.

Akihutubia wadau katika sekta ya elimu katika Taasisi ya Kuandaa Mitalaa Nchini (KICD) juzi Profesa Magoha alisema wale waliotunga mitihani ya KCPE na KCSE walitilia maanani hali kwamba wanafunzi walikaa nyumbani kwa muda mrefu kutokana na janga la Covid-19.

“Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) imezingatia kwamba shule zilifungwa kwa kipindi kirefu ilipotunga mitihani ya KCPE na KCSE. Kwa hivyo, tuko na matumaini kuwa watoto wetu watafanya vizuri,” akasema.

Profesa Magoha hata hivyo, ameonya wale watakaothubutu kushiriki udanganyifu kwamba mikakati mikali imewekwa kuzuia uovu huo. “Tumepata habari kwamba wengine wanapanga

You can share this post!

Didmus Barasa asema amegura siasa za wilbaro kuunganisha...

Haaland aokotea Dortmund pointi moja dhidi ya Cologne...