Hatma ya Sakaja kujulikana Julai 6

Hatma ya Sakaja kujulikana Julai 6

NA RICHARD MUNGUTI

HATMA ya Seneta Johnson Sakaja kuwania ugavana iko njia panda hata baada ya mahakama kuu kukataa ombi la kusimamisha kuchapishwa kwa kura.

Jaji Antony Mrima alikataa kusitisha kuchapishwa kwa kura za Ugavana Nairobi akisema “agizo kama hilo litavuruga kaunti nyingine 46 ambazo wawaniaji wake hawana shida ya kuhitimu kwa shahada ya digrii.”

Jaji Mrima aliamuru kesi mpya ya kubaini ikiwa Sakaja amehitimu kuwania Ugavana au la isikizwe Julai 4,2022.

Jaji huyo alifahamishwa na mpiga kura Bw Dennis Gakuu Wahome kwamba Tume ya Elimu ya Juu (CUE) imefutilia mbali digrii ya Sakaja kutoka Chuo Kikuu cha Team, Uganda baada ya kupokea ushahidi mpya.

Kufuatia ushahidi mpya kwamba Chuo Kikuu cha Team hakikuwa kikifunza masuala ya usimamizi (sayansi) 2016, Bw Wahome anaomba mahakama kuu iamuru jina la Sakaja ling’olewe kutoka karatasi za kura.

Bw Wahome aliomba Jaji Mrima aamuru uchapishaji wa kura za ugavana kaunti ya Nairobi usitishwe.

Ombi hilo lilipingwa vikali na mawakili wa tume ya uchaguzi na mipaka (IEBC) ikisema “agizo la kusitisha uchapishaji wa kura utakuwa na madhara makubwa kwa zoezi hilo la uchapishaji kura.”

Bw Wahome amedumisha Sakaja hana digirii na ile aliwasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi Nairobi Albert Gogo kabla ya kuidhinishwa kuwania Ugavana Nairobi ni feki.

Mawakili Elias Mutuma, Adrian Kamotho na Duncan Oktach walipinga vikali ombi la Wahome la kuliondoa jina la Sakaja katika karatasi za kura za ugavana Nairobi wakisema “aliruhusiwa na kamati ya kuamua mizozo ya uteuzi (DRC) kuwania ugavana Nairobi.”

Mabw Mutuma, Kamotho na Okatch walisema hakuna agizo kutoka mahakama kuu ama mahakama ya rufaa la kubatilisha uamuzi wa DRC kwamba Sakaja amehitimu kwa shahada ya digrii kuwania Ugavana Nairobi.

IEBC ilieleza Jaji Mrima kwamba ombi kura sizichapishwe litapelekea zoezi lote la kuchapisha kura za kaunti 47 kufutiliwa mbali.

Jaji huyo alikubaliana na msimamo wa IEBC kura ziendelee kuchapishwa kwa kuwa kusimamisha sasa kutasababisha mtafaruku.

“Naamuru wahusika wote katika kesi hii wawasilishe ushahidi kabla sijatoa uamuzi mapema wiki ijayo,” akaamuru Jaji Mrima.

  • Tags

You can share this post!

Mgombea udiwani ashtakiwa kwa kumwandalia mzee safari ya...

Guendouzi sasa mali rasmi ya Marseille

T L