Habari Mseto

Hatua iliyopigwa Kenya kuongeza idadi ya vifaru yasifiwa

October 16th, 2019 1 min read

Na MAGDALENE WANJA

SHIRIKA la International Rhino Foundation limetambua hatua kubwa ya kiteknolojia iliyopigwa Septemba nchini Kenya, ya upandikizaji – Assisted Reproductive Technology (ART) – kama mojawapo ya hatua kuu duniani za kusaidia katika ongezeko la idadi ya vifaru duniani.

Teknolojia hiyo ya ART ilifanyika baada ya watafiti kuyachukua mayai kutoka kwa vifaru wawili katika hifadhi ya wanyamaporu ya Ol Pajeta Nanyuki.

Katika ripoti yao ya mwaka 2019, shirika hilo la IRF limetangaza ongezeko la idadi ya vifaru duniani kwa muda wa miaka 10 iliyopita ambapo idadi yake ni 27,300.

“Hatua kuu zimepigwa kwa muda wa miaka 10 iliyopita katika spishi mbalimbali za vifaru, kama vile wale weusi katika bara la Afrika, na wale wenye pembe moja – greater one-horned – ambao walikuwa idadi chini ya 100 ila kufikia sasa kuna vifaru zaidi ya 3,600,” ilisema ripoti hiyo.

Kuhifadhi vifaru

Ripoti hiyo ilizitambua nchi kama vile India na Nepal ambazo zimeonyesha juhudi kuu katika kuhifadhi vifaru.

Hatua zingine ambazo zimechangia katika ongezeko la vifaru kuwepo kwa sharia kali katika mbuga mbalimbai za wanyama ambazo zimewapa ulnzi vifaru.

Hata hivyo, suala la uwindaji haramu limesalia kuwa changamoto kuu katika juhudi za kuhifadhi vifaru.