Habari za Kitaifa

‘Hatuajiri tena’: Serikali kuzima utoaji kazi katika utumishi wa umma

June 15th, 2024 1 min read

Na MWANDISHI WETU

SERIKALI itasimamisha uajiri katika sekta ya umma kama njia ya kupunguza matumizi ya serikali.

Akisoma Bajeti ya 2024/2025 jana, Waziri wa Fedha Profesa Njuguna Ndung’u alisema hatua hiyo inalenga kuthibiti bajeti.

“Hatua za kudhibiti matumizi ni pamoja na kusimamishwa kwa wafanyakazi wote wapya kwa mwaka mmoja ujao,” waziri alisema.

Vile vile, alisema kwamba, serikali itasitisha ununuzi wa samani za ofisi katika ofisi zote za serikali kwa mwaka mmoja.

Profesa Ndung’u pia alitangaza kusimamishwa kwa urekebishaji na ukarabati wa ofisi za umma.

Afisa kadhaa za serikali zilikuwa zimeomba pesa za kununua samani mpya na ukarabati ambao waziri alisema hautakubaliwa katika mwaka huu wa kifedha kama hatua ya kupunguza matumizi.

Serikali pia itapunguza ununuzi wa magari mapya katika mwaka ujao wa matumizi ya serikali utakaoanza Julai 1.

“Tunapaswa kuhakikisha kuwa rasilimali zetu adimu zinatumika kwa njia bora na nzuri,” alisema

Serikali pia itakuwa ikikagua orodha ya malipo.

“Tutapunguza matumizi ya serikali kwa kutumia teknolojia na hii itahusisha matumizi ya Wi-Fi na barua pepe kwa mawasiliano bora.