Habari Mseto

Hatuwezi kuiba chupa za maji, washukiwa wajitetea

May 22nd, 2018 1 min read

Kutoka kushoto: Jones Musyoka, Duncan Mungai Karanja na Daniel Kitheka Kitema walipofikishwa mahakamani Mei 21, 2018. Picha/ Richard Munguti

Na RICHARD MUNGUTI

WAFANYAKAZI wa kampuni ya kuuza maji Jumatatu walishtakiwa kwa wizi wa chupa 1,200 za kuweka maji zenye thamani ya Sh1.2 milioni.

Mabw Jones Musyoka, Duncan Mungai Karanja na Daniel Kitheka Kitema walikanusha mashtaka mawili ya wizi wa chupa za kuweka maji za lita 18.9 za kampuni ya Sunny River Limited.

Washtakiwa walikana waliiba mitungi hii ya kuweka maji  kati ya Machi 31 na Mei 19 , 2018.

Mnamo Mei 19 washtakiwa walikana walipatikana walipatikana na mitungi 69 ya kuweka maji wakijua imeimbwa ama kupatikana kwa njia isiyo halali.

Wote waliomba korti iwaachilie kwa dhamana.

Kiongozi wa mashtaka Bw Solomon Naulikha hakupinga ombi hilo.

Bw Andayi aliamuru washukiwa hao walipe dhamana ya Sh100,000 pesa taslimu hadi Julai 3 kesi itakaposikizwa.