Kimataifa

Helikopta ya Rais wa Iran yaanguka muda mfupi baada ya kupaa

May 19th, 2024 1 min read

NA MWANDISHI WETU

HALI ya Rais wa Iran Ebrahim Raisi bado haijajulikana kufuatia mkasa wa ajali ya ndege katika mpaka wa Iran na Azerbaijan, Jumapili jioni.

Kulingana na ripoti za mashirika, ndege hiyo ya helikopta ilianguka muda mfupi baada ya kupaa angani na juhudi za uokoaji zingali zinaendelea ingawa zimekumbwa na hali mbaya ya hewa.

Waziri wa Mashauri ya Ndani amethibitisha kuhusika kwa Rais Raisi kwenye mkasa huo, huku runinga ya kitaifa ikionyesha wananchi wakifanya sala kumuombea kiongozi wa nchi.

Habari zaidi ni kadiri tunavyozipokea…