Michezo

Henry Omino atajwa kocha mkuu Kisumu All Stars

June 24th, 2019 1 min read

Na JOHN ASHIHUNDU

Kisumu All Stars ambayo majuzi ilifuzu kwa Ligi Kuu ya Kenya (KPL) imemuajiri Henry Omino kuwa kocha wake mkuu.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa kocha huyo kurejea kwenye ligi hiyo inayodhaminiwa na SportPesa baada ya kutimuliwa na Western mnamo 2017.

Omino amechukuwa nafasi ya Andrew Oroka ambaye sasa atakuwa meneja mpywa wa timu hiyo, huku Farncis akihudumu kama kocha msaidizi wa Omino mwenye umri wa miaka 53.

Habari zaidi zilisema kadhalika klabu hiyo inatafuta wachezaji kadhaa wenye uzoefu wa mechi kubwa kwa ajili ya msimu mpya utakaoanza mwezi ujao.

Mtihani wa kwanza kwa Omino utakuwa wakati timu hiyo itakapokutana na Ulinzi kwenye mechi yao ya kwanza ugani Moi Stadium, Kisumu mnamo Agosti 31, kabla ya kukutana na KCB mjini Machakos katika uwanja wa Kenyatta Stadium.

Katika mechi yao ya Omino atapanga vijana wake dhidi ya timu yake ya zamani, Western Stima kabla ya kuvaana na Posta Rangers na baadaye Bandari FC.