Hii ndoto ya dereva chipukizi Yuvraj

Hii ndoto ya dereva chipukizi Yuvraj

Na JOHN KIMWERE

YUVRAJ Rajput ni chipukizi mwenye umri wa miaka 11 anayelenga kuwa mmoja wa madereva bora nchini Kenya.

Kinachomsisimua zaidi katika mbio za magari ni kupaisha.Yuvi, anavyofahamika kinda huyu kwa jina la utani, tayari ni bingwa mara mbili wa kitaifa wa mbio za magari na vigari maarufu kama Autocross, akishiriki kitengo cha vigari cha Bambino.

Alizoa taji lake la pili la kitaifa Novemba 14, wakati wa duru ya nane ya Autocross iliyodhaminiwa na benki ya KCB, katika uwanja wa Twisty Corners katika Kaunti ya Kiambu.Alikamata nafasi ya pili nyuma ya Amaan Ganatra. Yuvi alikuwa amepata alama za kutosha kushinda msimu.

Ikisalia raundi moja, ambayo itafanyika Desemba, chipukizi huyu amezoa pointi 188 dhidi ya mpinzani wa karibu Karamveer Singh Rooprai (153).Yuvi alitwaa taji lake la kwanza la kitaifa la Bambino mwaka 2019, huku mashindano ya 2020 yakifutiliwa mbali kwa sababu ya corona.

Mwaka 2022 anajitosa katika kitengo cha juu cha chipukizi cha 2WD Non Turbo.Aliambia Taifa Leo kuwa babake Kirit Rajput amemuahidi kigari kipya chenye nguvu mara tatu kuliko cha sasa ,ikiwa atapita mtihani wake.“Ndoto yangu ni kushiriki Mbio za Magari Duniani (WRC) ama mbio za langalanga (Formula 1).

Ila masomo pia nayapa kipaumbele,” alieleza mpenzi huyo pia wa soka, uendeshaji wa baiskeli, gofu na mpira wa vikapu.Magwiji Baldev Chager, Quentin Mitchell na Eric Bengi ni baadhi ya madereva waliokuza talanta zao kupitia Karting na Autocross kabla ya kuwa madereva mahiri.

Nilianza fani hii kwa kuendesha vigari katika mbio za Karting kwenye barabara za lami. Naamini nitakuwa tayari kabisa mwaka ujao kwa mashindano ya 2WD Non Turbo yanayoleta pamoja madereva walio kati ya umri wa miaka 12 na 16,” anasema.

Magwiji Baldev Chager, Quentin Mitchell na Eric Bengi ni baadhi ya madereva waliokuza talanta zao kupitia Karting na Autocross kabla ya kuwa madereva mahiri.Yuvraj anahitimisha kwa kusema, “Masomo kwangu nayapatia kipaaumbele.

Kwa hivyo, napata kufanya mazoezi ya kuendesha vigari wakati sina kazi ya shule. Mpenzi huyo pia wa soka, uendeshaji wa baiskeli, gofu na mpira wa vikapu ana dada mdogo Kiana Rajput ambaye pia yuko pua na mdomo kutawazwa bingwa wa kitengo cha Pee Wee mwaka 2021.

You can share this post!

Ari ya kisasi ilimsukuma kwa ndondi

Origi awakomboa Reds tena

T L