Himizo Mkaguzi ashirikishe umma huku akizindua nakala ya Kiswahili

Himizo Mkaguzi ashirikishe umma huku akizindua nakala ya Kiswahili

NA CHARLES WASONGA

MKAGUZI Mkuu wa Hesabu za Serikali Nancy Gathungu, ametakiwa kuendeleza mpango wa ushirikishaji wa umma katika ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma katika serikali kuu na za kaunti.

Bi Gathungu amehimizwa kushirikiana na vyombo vya habari ili kuhakikisha kuwa ripoti za ukaguzi wa pesa za umma ambazo hutolewa na afisi yake kila mwaka, zinawafikia watu wote.

Ushauri huu ulitolewa Jumatano na wadau mbalimbali, katika kikao cha mashauriano kati ya afisi hiyo na Chama cha Wahariri Nchini (KEG) katika mkahawa mmoja jijini Nairobi.

Kikao hicho pia kilishuhudia uzinduzi wa nakala ya kwanza ya ripoti ya ukaguzi wa matumizi ya fedha iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.

“Afisi ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inafaa kupongezwa kwa kuchukua hatua mahsusi ya kutafsiri ripoti ya ukaguzi kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wanaelewa yaliyomo kwenye ripoti hizo,” akasema Bw Charles Kichere, Mdhibiti wa Bajeti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali katika Jamhuri ya Tanzania.

Bw Kichere, ambaye alikuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi huo, pia alisema ripoti za ukaguzi zilizotafsiriwa kwa Kiswahili zitaimarishaji uwajibikaji katika matumizi ya fedha za serikali.

“Hii ni kwa sababu wananchi watakuwa na uwezo uelewa mpango kuhusu jinsi pesa zao zinavyotumiwa katika ngazi mbalimbali za utawala,” akaongeza.

Kwa upande wake rais wa KEG Churchil Otieno alimhakikishia Bi Gathungu kwamba vyombo habari vitafanya kazi kwa ukaribu na afisi yake ili kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya mali ya umma.

You can share this post!

Jumla ya watu 55 wanataka kuwania urais

Gachagua amtetea Ruto kwa kumteua mgombea mwenza

T L