NA WINNIE ATIENO
WAGONJWA wa fistula wametakiwa kwenda katika vituo vya afya kupokea matibabu badala ya kujificha nyumbani.
Afisa wa matibabu katika kituo cha afya cha Bura, Kaunti ya Tana River, Bw Charo Mwambire, aliwahakikishia kuwa hali ya fistula inaweza kutibiwa.
Kadhalika alionya Wakenya dhidi ya unyanyapaa kwa wagonjwa wa fistula.
Aliongea siku moja baada ya Kenya kujiunga na ulimwengu kuadhimisha siku ya fistula duniani ambapo wananchi walihamasishwa kuhusu ugonjwa huo, matibabu na namna unyanyapaa imeathiri wagonjwa kutafuta matibabu.