Hisia mseto Zuma akiachiliwa huru kwa msamaha

Hisia mseto Zuma akiachiliwa huru kwa msamaha

Na MASHIRIKA

PRETORIA, Afrika Kusini

RAIS wa Afrika Kusini amekaribisha uamuzi wa kumwachilia huru aliyekuwa rais Jacob Zuma kupitia msamaha kutokana na hali yake ya afya.

Ramaphosa alimtakia Zuma afueni ya haraka alipokuwa akitoa kauli yake ya mwisho katika kikao na kamati kuu ya kitaifa ya chama kinachotawala cha ANC.

“Tunakaribisha hilo. Tumesikia kwamba hajihisi vyema na tungependa kumtakia afueni ya haraka anaporejeshwa nyumbani kwake ili awe na wapendwa wake,” alisema.

Idara ya Huduma za Kurekebisha Tabia ilithibitisha wikendi iliyopita kwamba Zuma ataachiliwa huru kutoka jela na kuhudumu muda uliosalia wa kifungo chake nyumbani kwake Nkandla.

Haikubainishwa anaugua ugonjwa upi lakini taarifa kutoka idara hiyo ilisema kuwa atakamilisha muda uliosalia wa kifungo chake katika jamii ambapo atahitajika kufuata masharti maalum.

“Hatua ya Zuma kuwekwa kwenye msamaha wa kimatibabu inamaanisha atakamilisha muda uliosalia wa kifungo chake katika mfumo wa kurekebisha jamii ambapo ni sharti afuate masharti fulani chini ya uangalizi hadi kifungo chake kitakapokamilika,” ilisema idara hiyo.

You can share this post!

Kigogo wa upinzani kusalia rumande jaji akijiondoa kesini

Laikipia yalipuka