Historia matokeo yakitua siku 3 baada ya usahihishaji

Historia matokeo yakitua siku 3 baada ya usahihishaji

Na Benson Matheka

HISTORIA iliandikishwa jana baada ya matokeo ya mtihani wa kidato cha nne (KCSE) kutolewa siku tatu baada ya zoezi la usahihishaji kukamilika.

Waziri wa Elimu Profesa George Magoha, alitimiza ahadi yake kwamba matokeo ya mtihani huo yangetolewa bila kucheleweshwa.

Prof Magoha alifunga zoezi la kutahini KCSE ya mwaka 2020 Ijumaa wiki jana na kuahidi kwamba matokeo yangetangazwa pindi yakiwa tayari.“Matokeo yakiwa tayari basi yako tayari na tutayatoa,” alisema na kuongeza kuwa yangetolewa kabla au Mei 10.

Matokeo ya mitihani ya kitaifa yamekuwa yakipigwa darubini kufuatia madai ya ufisadi uliofanya yacheleweshwe miaka ya awali.

Waziri alisema kwamba kutolewa mapema kwa matokeo ya mitihani kutazuia baadhi ya wakuu na wamiliki wa shule kushirikiana na maafisa wa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) kupendelea shule zao.

Baraza hilo pia limekumbatia teknolojia katika hatua za kuzuia ufisadi katika matokeo ya mitihani.

 

You can share this post!

Wasichana wazidi idadi ya wavulana katika KCSE Kwale

Madiwani 78 wakataa mwaliko wa kukutana na Moi