Kimataifa

Historia ndoa kudumu dakika 3 pekee!

February 7th, 2019 1 min read

MASHIRIKA Na PETER MBURU

HISTORIA iliwekwa duniani baada ya wanandoa nchini Kuwait kushangaza ulimwengu kwa kutalikiana dakika tatu tu baada ya kufunga ndoa, bi harusi alipovua nguo wakati wa sherehe.

Ndoa yao inasemekana kuwa fupi zaidi katika historia ya ndoa nchini humo, kwani walipokea vyeti vya talaka hata kabla ya kuondoka ukumbi ambapo walifanyia harusi.

Wawili hao wanasemekana kuwa walikuwa wametia saini cheti cha ndoa tu na bado walikuwa mbele ya jaji aliyewaunganisha, wakati bi harusi kimakosa alianza kuvua nguo walipokuwa wakitoka nje.

Alipokosolewa kwa kufanya hivyo, mwanamke huyo alizua rabsha na kumtaka jaji huyo kuvunja ndoa yao ya dakika chache, papo hapo. Ni dakika tatu pekee zilikuwa zimekamilika tangu waunganishwe.

Kisa hicho kiliibua hisia za huruma kwa mwanamke huyo kwenye mitandao ya kijamii, huku watu wengi wakisema kuwa alikuwa anataka ndoa hiyo ivunjwe.

“Ikiwa anafanya hivi (mwanamume) mwanzoni, afadhali awachwe,” mtu mmoja alisema.

Wengine walidai kuwa ndoa hiyo haingekuwa na heshima.