Hofu Kaunti ikikosa chanjo dhidi ya Covid

Hofu Kaunti ikikosa chanjo dhidi ya Covid

Na IAN BYRON

MAAFISA wa afya katika Kaunti ya Migori wameibua hofu kuhusu uhaba mkubwa wa chanjo ya corona huku visa vya maambukizi vikiongezeka.

Afisa Mkuu wa Afya katika Kaunti hiyo, Bi Pauline Amollo, Alhamisi aliambia Taifa Leo kwamba idara ya afya tayari imelemewa na wananchi wanaotaka chanjo.

“Tumeshuhudia ongezeko la watu wanaotaka chanjo lakini tunakabiliwa na uhaba mkubwa wa dozi wa kukidhi hitaji hili. Sasa tunasubiri dozi nyingine kutoka Serikali ya Kitaifa kwa sababu hata hifadhi ya Kisumu inakabiliwa na upungufu,” Bi Amollo akasema.

Afisa huyo alisema dozi ambazo kaunti ilipokea awali ziliisha juzi baada ya watumishi wa umma kujitokeza kwa wingi kupewa chanjo. Hata hivyo, alihimiza wakazi kuwa wavumilivu.

You can share this post!

Moussa Sissoko aondoka Spurs na kujiunga na Watford kwa...

KASHESHE: Akanusha kuvaa vigodoro