Hofu msongamano wa chanjo huenda uibue maambukizi

Hofu msongamano wa chanjo huenda uibue maambukizi

Na KENYA NEWS AGENCY

WALIMU wameibua hofu ya ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona miongoni mwao kutokana na msongamano mkubwa ambao umekuwa ukishuhudiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Bungoma ili kupata chanjo.

Katibu wa KNUT wa Bungoma Kusini, Bw Ken Nganga, alisema kuwa japo Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dkt Anthony Walela aliwahakikishia walimu kuwa chanjo inapatikana katika hospitali zote za kata na sita za kibinafsi, ni hospitali ya hiyo ya rufaa pekee na mbili za kibinafsi zinazotoa chanjo.

Akizungumza na wanahabari katika Kaunti ya Bungoma, Bw Nganga alisema kuwa Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) na serikali hazifai kuwalazimisha walimu kupata chanjo.

“Serikali haifai kumlazimisha mtu yeyote kupata chanjo. Kila mmoja anafaa kuchanjwa kwa hiari yake,” akasema Bw Nganga.

Hata hivyo, aliwahimiza walimu wote wajitoe ili wapate chanjo.

You can share this post!

TSC yapata ngao kuzuia walimu kujihusisha na ubodaboda

Madiwani wataka kupewa bunduki ‘kupambana’ na polisi