Habari Mseto

Hofu Siaya padre akieneza coronavirus

March 24th, 2020 1 min read

WAANDISHI WETU

HOFU imetanda katika Kaunti ya Siaya, baada ya padre wa Kanisa Katoliki aliyetangamana na wakazi kwa siku kadhaa kupatikana ana virusi vya corona.

Padre huyo alikuwa amerudi nchini kutoka Italia ambako janga la corona limechacha. Hapo jana Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alithibitisha kuwa padre huyo alikuwa miongoni mwa watu wanane waliothibitishwa kuugua mnamo Jumapili.

Mapadre zaidi ya 100 na watawa wapatao 30 waliopokea sakaramenti kutoka kwa padre huyo wakati wa ibada ya Juma- pili sasa wanaishi kwa hofu kuwa huenda aliwaambukiza virusi vya corona.

Wasiwasi pia umezuka eneo la Ambira ambako padre huyo aliongoza ibada ya mazishi mnamo Machi 14, kisha akaenda kulala kwa kasisi mwenzake.

Waziri Kagwe alithibitisha kuwa kasisi huyo amelazwa katika Hospitali ya Mbag- athi jijini Nairobi Katika kaunti ya Uasin Gishu, madiwani saba wamejitenga baada ya kurudi nchini

mnamo Machi 15 kutoka ziara ya kikazi ji- jini Dubai. Kulingana na Spika wa Bunge la Uasin Gishu David Kiplagat, madiwani wengine wanane tayari walijitenga kwa siku 14 na kisha kujumuika na familia zao baada ya kubainika hawakuwa wamembukizwa.

Baadhi ya madiwani katika Kaunti ya Kilifi pia wamelazimika kujitenga baada ya kutangamana na naibu gavana Gideon Saburi anayeugua ugonjwa wa corona.

Hapo jana kikosi cha kukabiliana na visa vya corona katika Kaunti ya Narok kilimlazimisha mwanamke wa umri wa miaka 59 kujitenga katika Hospitali ya Rufaa ya Narok. Mwanamke huyo alirejea nchini majuzi kutoka Sweden.

Kulingana na Kamishna wa Kaunti ya Narok Samuel Kimiti, serikali inasaka waumini wa kanisa alilohudhuria pamoja na watu wa familia yake waliomlaki alip- owasili kutoka Sweden.

Waumini waliotangamana naye wakati wa ibada ya Jumapili iliyopita pia wana- sakwa katika juhudi za kutaka kuzuia maambukizi zaidi.