Hofu uvamizi wa nzige unapunguza asali

Hofu uvamizi wa nzige unapunguza asali

Na Geoffrey Ondieki

UVAMIZI wa nzige nchini sasa unaangamiza nyuki na kuchangia kupungua kwa uzalishaji wa asali katika kaunti zilizoathirika, wanasayansi wameonya.

Kando na makundi na wadudu hao kufyeka matawi na miti na nyasi misituni na kutishia uzalishaji wa asali, kemikali ambayo serikali inatumia kuangamiza nzige hao pia inaua nyuki na wadudu wengine.

Mtaalamu wa mimea ya kilimo, Timothy Okwaro anasema kemikali inayonyunyiziwa nzige pia huangamiza ndege na wadudu wengine wenye manufaa na misitu.

Katika kaunti ya Samburu ambapo asilimia 20 ya wakazi wanategemea uzalishaji asili kama kitega uchumi kikuu, nzige wamevamia misitu ya Kirisia na Ndoto Nyiro.

Data kutoka kwa Chama cha Wafugaji Nyuki Samburu inaonyesha kuwa kiwango cha uzalishaji asali umepungua kwa kiwango kikubwa kote Samburu.Ingawa unyunyiziaji dawa unaweza kudhibiti nzige hao, mwenyekiti wa chama hicho John Lelesiit sasa ameingiwa na hofu kwamba kemikali hizo zinaangamiza nyuki katika kaunti hiyo.

You can share this post!

Nyong’o apigwa kumbo na wandani wake wa zamani

Amri ya kusitisha mikutano yapoza joto la kisiasa