Habari Mseto

Hofu watu wengi zaidi huenda wakaangamia kwa corona Afrika Kusini

June 18th, 2020 1 min read

NA MASHIRIKA

CAPE TOWN

Nchi ya Afrika Kusini ilirekodi visa 2,801 kwa siku moja huku hofu ikizukwa kuwa kuna uwezekano wa watu wengi kuafariki, Wizara ya Afya nchini humo ilisema Jumatano.

Idadi ya visa vya corona sasa imepanda hadi 76,334. Watu wengine 57 wamefariki kutokana na virusi vya corona huku idadi ya waliofariki ikifikia 1625.

Waziri wa Afya Zweli Mkhize alionywa kwamba kuna uwezekano wa nchi kushuudia vifo vingi kutokana na corona siku za usoni kutokana na ongezeko la maambukizi.

Waziri wa Maendeleo ya Kijamii Lindiwe Zulu akihutubia wananchi alisema kwamba maswala ya kujizuia yako mikononi mwa wananchi kulingana na mienendo yao huku akiwahimiza wananchi kujikinga na virusi vya corona ili kupunguza kusambaa kwake.

“Kubadilisha tabia kunahusu kuvaaa barakoa, kuosha mikono, kuweka umbali wa mita moja,” alisema Mkhize .

“Ili kukabiliana na virusi hivi, si serikali tu inajukumika, pia ni ni tabia ya kila mmoja,” alisema Mhize.

Tangu ugonjwa huo uingie nchini humo hapo Machi, nidhamu na ushirikiano umewezesha Afrika Kusini kuthibiti ugonjwa huo.