Hofu ya maafa mvua ikizidi maeneo mbalimbali nchini

Hofu ya maafa mvua ikizidi maeneo mbalimbali nchini

BENSON MATHEKA na DIANA MUTHEU

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha sehemu kadhaa nchini imeathiri shughuli huku hofu ya kuzuka kwa maradhi ikiongezeka.

Shirika la Msalaba Mwekundu nchini (KRC) lilisema watu wanaendelea kukosa makao baada ya makazi yao kufurika maji hasa katika eneo la Pwani.

Shirika la Taifa la Kukabiliana na Mikasa (NDOC) lilisema kuwa kaunti zilizoathiriwa zaidi ni Nairobi, Mombasa, Turkana, Wajir, Mandera, Marsabit na Tana River.

Baadhi ya barabara jijini Nairobi na Mombasa zilifuruka maji na kufanya wakazi kushindwa kusafiri.

Katika kaunti ya Mombasa, mvua kubwa ilisababisha mafuriko katika sehemu mbalimbali na kulemaza usafiri na shughuli za kawaida za wakazi.Watabiri wa hali ya hewa walisema kuwa mvua hii itaendelea kunyesha kwa muda wa saa 30.

Kulingana na Kamishna wa Kaunti ya Mombasa, Gilbert Kitiyo, magari kadhaa yalisombwa na maji huku barabara moja katika eneo la Jomvu ikiharibiwa.

Akizungumza na Taifa Leo, Bw Kitiyo alithibitisha kuwa hakuna majeruhi lakini akahakikishia wananchi kuwa ofisi yake iko makini kufuatilia hali itakavyokuwa.

“Wakazi wanapaswa kujiepusha na maeneo karibu na ufuo wa bahari na pia kuondoka katika sehemu zinazokumbwa na mafuriko,’ Bw Kitiyo alisema.Utabiri wa hali ya hewa unaonyesha kwamba mvua itaendelea kunyesha hadi wiki ya tatu ya mwezi wa Desemba.

Kamishna huyo pamoja na watabiri wa hali ya hewa waliwaonya watalii na wavuvi dhidi ya kuingia baharini.Kaunti zilizoathiriwa zaidi katika mkoa huo ni Mombasa na Kilifi. Jana katika kaunti ya Mombasa, mvua ilinyesha kwa muda wa saa 24.

Kaunti za Kwale, Taita-Taveta na Lamu, mvua ni kidogo.Maeneo yaliyoathiriwa zaidi ni Bombolulu, Likoni, Mshomoroni, Jomvu, Kiembeni na katikati ya mji wa Mombasa (CBD).

Barabara ya Moi, Mombasa ilifurika na majengo ya biashara kando ya barabara yaliingia maji.

Shughuli katika vituo kadhaa vya mafuta kando ya barabara ya Jomo Kenyatta zililemazwa kwa sababu zilikuwa zimefurika.Maafisa wa afya katika mkoa huo walionya kwamba maji ya mvua yanaweza kusababisha kuzuka kwa magonjwa yanayotokana na

You can share this post!

#JkuatLivesMatter: Polisi waliopiga mwanachuo watemwa

WASIA: Patiliza changamoto inayokukabili iwe ngazi katika...

adminleo