Michezo

Homeboyz majogoo wa Prinsloo Sevens

July 23rd, 2018 2 min read

Na GEOFFREY ANENE

MABINGWA wa Raga ya Kitaifa ya wachezaji saba kila upande mwaka 2016, Homeboyz walianza msimu 2018 kwa kushinda duru ya ufunguzi ya Prinsloo Sevens mjini Nakuru, Jumapili.

‘Madeejay’ hawa walipepeta mabingwa wa mwaka 2007, 2008, 2010 na 2011 Mwamba kwa alama 19-12 katika fainali kali uwanjani Nakuru Athletic.

Homeboyz, ambayo pia mara ya mwisho ilikuwa imeshinda Prinsloo Sevens ilikuwa mwaka 2016, ililemea Mwamba kupitia miguso ya Bush Mwale, Alvin Otieno na Mark Wandeto na mikwaju miwili kutoka kwa Michael Wanjala. Mwamba ilifunga miguso yake miwili kupitia Daniel Taabu na Joel Izuga.

Mabingwa wa Prinsloo mwaka 2017 KCB walikamilisha ziara yao ya kaunti ya Nakuru katika nafasi ya nne. Walipepetwa japo pembamba 12-10 na mabingwa wa kitaifa mwaka 1999, 2000, 2001 na 2004 Impala Saracens katika mechi ya kutafuta mshindi wa medali ya shaba. Wanabenki wa KCB waliibuka mabingwa wa raga hizi za kitaifa mwaka 2013 na 2014.

Matokeo ya Prinsloo Sevens 2018:

Fainali Kuu

Homeboyz 19-12 Mwamba

Mechi ya kutafuta nambari 3 na 4

Impala Saracens 12-10 KCB

Nusu-fainali Kuu

Homeboyz 29-12 Impala Saracens

Mwamba 10-5 KCB

Robo-fainali Kuu

Nakuru 12-14 Impala Saracens

Kabras Sugar 5-10 Homeboyz

Mwamba 5-0 Kenya Harlequins

Menengai Oilers 10-12 KCB

Nusu-fainali ya kutafuta nambari 5 hadi 8

Kabras Sugar 21-26 Nakuru

Kenya Harlequins 10-5 Menengai Oliers

Fainali ya kupata nambari 5 na 6

Nakuru 17-22 Kenya Harlequins

Robo-fainali ya Challenge Trophy

Mean Machine 12-10 Blak Blad

Nondies 19-14 Mombasa

Strathmore Leos 38-0 Kisumu

Catholic Monks 31-0 Webuye

Nusu-fainali ya Challenge Trophy

Mean Machine 12-7 Nondies

Strathmore Leos 33-19 Catholic Monks

Fainali ya Challenge Trophy

Mean Machine 21-14 Strathmore Leos

Nusu-fainali ya mechi ya kutafuta nambari 13 hadi 16

Blak Blad 31-12 Mombasa

Kisumu 14-12 Webuye

Fainali ya kupata nambari 13 na 14

Blak Blad 22-7 Kisumu

Ratiba ya Raga ya Kitaifa mwaka 2018

Julai 21-22: Prinsloo Sevens (Nakuru Athletic Club)

Julai 28-29: Sepetuka Sevens (Eldoret Sports Club)

Agosti 18-19: Kabeberi Sevens (Machakos)

Agosti 25-26: Driftwood Sevens (Mombasa Sports Club)

Septemba 8-9: Dala Sevens (Mamboleo Showground Kisumu)

Septemba 15-16: Christie Sevens (RFUEA Ground Nairobi)