Habari Mseto

Hospitali za umma 001 kutoa matibabu ya afya ya akili

March 1st, 2024 1 min read

NA WINNIE ATIENO

SERIKALI ya Kaunti ya Mombasa itaanza kutoa huduma za afya ya akili katika hospitali kadhaa za umma.

Hatua hii inanuia kupunguza msongamano katika hospitali maalum ya wilayani Port Reitz ambayo ndio ya kipekee inayotoa huduma za afya ya kiakili eneo la Pwani.

Port Reitz ndio hospitali kubwa zaidi baada ya Mathari iliyoko Nairobi ambayo inatoa huduma hizo za matibabu ya kiakili.

“Kamati ya huduma za afya ya akili imeanza mikutano kujadili namna ya kupunguza msongamano katika hospitali ya Port Reitz. Hii itafanywa kwa kuongeza huduma hizo katika hospitali zengine za umma kaunti ya Mombasa,” serikali hiyo ya kaunti ilisema.

Serikali hiyo ya kaunti inayoongozwa na Gavana Abdulswamad Nassir ilisema pia imeweka mikakati ya kuongeza idadi ya wahudumu wa afya wa kiakili kukabiliana na ugonjwa huo.