Makala

VIDUBWASHA: HTC yarejea, mara hii yatoa simu za maana kabisa (HTC U19e na HTC Desire U19 Plus)

June 18th, 2019 1 min read

Na LEONARD ONYANGO

BAADA ya kimya cha muda mrefu, wengi walidhani kampuni ya simu ya High Tech Computer (HTC) ya nchini Taiwan imefunganya virago na kuondoka kabisa katika soko la simu.

HTC ilizindua simu zake, HTC U12 Life na U12 Plus mara ya mwisho mwanzoni mwa 2018.

Lakini kampuni hiyo imewaacha wengi vinywa wazi baada ya kuzindua ghafla simu mpya mbili, HTC U19e na HTC Desire U19 Plus ambazo huenda zikatamba katika soko la simu.

Simu ya HTC U19e ina kamera mbili nyuma za megapikzeli 24MP na 2MP.

HTC Desire U19 Plus ina kamera tatu nyuma za megapikzeli 13MP, 8MP na 5MP.