Habari Mseto

Huddah sasa akiri kuwezwa na uhodari kwa kidume kipya chumbani

August 29th, 2018 1 min read

Na PETER MBURU

MSOSHALAITI Huddah Monroe hatimaye amepata mpenzi, na sasa anataka kila mtu duniani ajue kuhusu uwezo wa dume lake kumtimizia uchu wa uroda chumbani.

Kwenye ujumbe katika Instagram Stories, Huddah alizungumzia kuhusu mpenzi wake wa mwaka mmoja sasa, ambaye alimtaja kuwa na ‘mchezo wa haja’.

Aliandika namna alivyowezwa na penzi la jamaa wake, japo kwa kinaya, akihofia kujitolea kuhifadhi penzi.

Kulingana naye, kujitokeza kwa jamaa mwenye gemu kali katika maisha yake ni ishara kuwa kuna wasakataji wazuri wa uroda kule nje, na hivyo hajui ikiwa ashikilie huyo ama ajitoe akawatafute.

Hadithi yake ya mapenzi inakuja wiki chache tu baada ya mwenzake Vera Sidika kutemwa na msanii Otile Brown, ambaye alikuwa ameonyesha ishara za kufunga pingu za maisha naye.

Sasa Huddah anasema amevunja sharia yake ya kwanza ya ‘kutowahi kunaswa kwa mapenzi’.

Mbeleni, alikuwa amemtambulisha mwanasoka mmoja kutoka Amerika kama mpenzi wake lakini baadaye akatangaza kuwa waliachana.

Kutoka wakati huo alisema aliamua kutowahi kuingia katika mapenzi yoyote ya kweli, kwani aliona yeye na ndoa ni maji na mafuta.

Lakini sasa anaonekana kuvunja amri yake mwenyewe, huenda kutokana na uhodari wa jamaa mpya aliyempata, lakini tumpe muda kabla ya kusherehekea kuwa mwishowe amepata kidume halisi cha kumwoa.